SoC01 Mitaji, Mikopo, Masoko na kuzalisha Faida kwa WanaJamiiForums

SoC01 Mitaji, Mikopo, Masoko na kuzalisha Faida kwa WanaJamiiForums

Stories of Change - 2021 Competition

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
MITAJI / MIKOPO

a) Wakopaji

Kuna wadau wengi katika Jamvi letu wanakuwa na uhitaji wa pesa kwa wakati Fulani lakini hawana pa kuzipata. Pia sababu watu hatujuani ni vigumu kuaminiana ila JF inaweza kutumika kama platform ya kuwaunganisha wahitaji (kwa kuwa-verify wakopaji) ili waweze kufanikisha hitaji lao

b) Wakopeshaji
Kuna watu pesa wanayo na wangependa kusaidia wengine, au kuzalisha pesa yao lakini hatari ya utapeli na kutokurudishiwa pesa yao au kujulikana (watu wanapenda kutokujulikana) inapelekea watu kuacha kukopesha / kuzalisha pesa zao. Lakini JF kama ikitumika kama medium / platform ya members kuweka pesa zao ili zifanyiwe kazi na wahitaji watu hao wanaweza kuzalisha / kusaidia bila Identity zao kuwa wazi Mfano Tukisema watu 4000 ambao ni wastani wa members online kila wakati kwa mwaka mtu akiamua kuwekeza 100,000/=; hizo ni 400,000,000/= (Milioni Mia Nne kwenye Kapu); kwahio wahitaji wenye matatizo na wataka mitaji wanaweza wakachukua kwa riba ndogo sana ili kufanikisha Shida zao za muda mfupi

MASOKO
Kuna wanajamii na makampuni mengi yanahitaji masoko, kuna wadau huwa wanakwenda kulima na kufuga na mwisho wa siku kukosa masoko. Ingawa kuna wahitaji wengi ila wanakosa Imani kwa kuogopa kutapeliwa, kujua ubora wa bidhaa husika, na kukosekana kwa urahisi wa kupata bidhaa.

JF pia inaweza ikatumika kama platform ya kuunganisha wahitaji kwa wao kuchukua mzigo (Kwa Jumla toka kwa Mwenye Mzigo) na kuhakikisha mnunuzi anapata bidhaa yake.

Mfano badala ya muuza Kuku mmoja kule Gamboshi kuuza kuku mmoja mmoja huku na kule anaweza akawa-process na kuwapack wote kwa jumla mpaka warehouse ya JF Dar ili wahitaji ambao watakuwa wameshatoa order tayari waweze kuchukua, vilevile kwa bidhaa kama korosho, dagaa n.k.

Pia kutokana na wingi wa wanajamii hata mimi nikiwa na order ya karanga mfano Kenya inakuwa rahisi kuwasiliana na JF waweze kunitafutia tani kadhaa za karanga. Au mtu yupo China au Marekani na mtu anahitaji Laptop Tanzania huyo mtu anatoa deposit kwa JF; na mdau wa China anatuma mzigo to JF ili muhusika aupate

FAIDA KWA WANAJAMIIFORUM
Je waliotoa laki zao watazipataje?

Ni vigumu ku-guarantee interest au huenda interest isiwe kubwa sana, lakini investment hiyo ikiwa mwisho wa mwaka mtoaji anapata fursa ya kuchagua bidhaa kwa bei ya jumla. Itasaidia kufanya platform iwe sustainable.

Mfano Badala ya kupata laki yake mtu anaweza kuchagua gunia mbili za mpunga, debe la mafuta, kurosho kiasi, maharage n.k. Au kwa wale wasio na familia au uhitaji wa Chakula wanaweza kwa pesa yao hio wakapata equipments / electronic gadgets ambazo huenda kwenye Retail Price zingekuwa ni mara tatu ya pesa yao.

Sababu JF itaweza ku-source hizo bidhaa kwa jumla tuko kwa wakulima na wauzaji wakubwa wataweza kuzipata hizo bidhaa kwa bei rahisi na kwa kuwauzia hawa waliochangia / watakaochangia kila mwaka bado wakapata faida. Kwa Platform itakuwa ni faida kubwa na watatumia mtaji kidogo na kuzidi kuzalisha Mtaji ambao utakuwa unakua mwaka hadi mwaka.

HITIMISHO
Kwa kufanya hivyo Hii Jamii itapiga hatua katika kusaidia:-
  1. Wahitaji wa pesa na mitaji kwa muda mfupi kwa kuwapatia pesa
  2. Kuwapatia masoko wauzaji
  3. Kuwapati faida ya bidhaa wawekezaji kwa kupata bidhaa za jumla mwisho wa mwaka; (Mtu anaweza akaweka bajeti kabisa kwamba natoa hii laki ili mwisho wa mwaka nipate mchele wangu, maharage au mahindi ya kula mwaka kesho) ; Au bidhaa yoyote itakayokuwepo kwa bei nafuu
 
Upvote 6
Baadhi wa Wadau ambao walishawahi kuomba mikopo humu ndani kwenye uzi tofauti tofauti ambao wangeweza kuwa catered for na huu mfumo (samahani kama takuwa nimeingilia privacy zao kwa kufufua uzi)


Ni kweli hapo wadau pesa inaweza isirudi kutokana na bahati nasibu za biashara za Tanzania ila inaweza ikawa pia kama msaada kuwatoa watu kwenye shida, mfano mtu amefiwa ameugua au amekwama anakimbilia hapa kukopeshwa; Na sababu dhumuni litakuwa ni kusaidia na sio mikopo umiza nadhani itakuwa a Good Deed
 
Wafujo

Nimeona unafikiria kuweka hata rehani vyeti vyako uweke mkopo; Nadhani kungekuwa na kitu kama hii ungekuwa mnufaika
 
Kabisa mkuu, ni kuendelea tu kupambana bila kujua hatma yako[emoji22]
Haipaswi kuwa hivyo, kungekuwa na alternative hata kama sio pesa kulingana na ujuzi wako mtu anakuunganisha kwenye project yake au kama kwenye database tunajua kwa uhakika fulani ana maharage tani kadhaa huko mbeya ingekuwa rahisi kwa wewe kutafuta mteja karibu ulipo ili upate mkate wako...

In short kwenye jamii ya watu wengi wenye mahitaji tofauti uwepo wa platform ya kuwaunganisha ni win win situation kwa wote, na bado watu tunaweza kuendelea kuwa anonymous na kutokujuana bali uwekezaji wetu na mitaji yetu ndio inajuana (pesa na bidhaa zinakuwa transparent kwenye mtandao)
 
Back
Top Bottom