Mitambo nane Bwawa la Nyerere yakamilika, bado mmoja

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mitambo nane kati ya tisa inayojengwa katika Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere, imekamilika na mmoja uliobakia utakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Kauli hiyo imetolewa bungeni jana Januari 31, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko wakati akichangia kwenye azimio la Bunge la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mwenyeji wa mkutano wa nishati Afrika (Mission 300) kwa mwaka 2025.

Amesema Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) unaojengwa kwa gharama ya Sh6.6 trilioni, mpaka kukamilika kwake, utazalisha megawati 2115 za umeme ingawa kwa sasa Tanzania inazalisha megawati 3,404.

Soma: Kamati ya Bunge: Bwawa la Nyerere litakamilika Juni 2024, Tsh. Trilioni 5.85 zimelipwa tayari
 
Mradi mmoja tu tirion 6 , bado ndege na fly over na tren ya umeme na stend ya kisasa kila mkoa

Mama Samia kakopa trion 36 kwa mda wa miaka mitatu lakin hakuna hata mladi mmoja aliofanya zaid ya kutembelea kila nchi na move ya loyal tour
 
Mitambo nane kati ya tisa inayojengwa katika Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere, imekamilika na mmoja uliobakia utakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Kauli hiyo imetolewa bungeni jana Januari 31, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko wakati akichangia kwenye azimio la Bunge la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mwenyeji wa mkutano wa nishati Afrika (Mission 300) kwa mwaka 2025.

Amesema Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) unaojengwa kwa gharama ya Sh6.6 trilioni, mpaka kukamilika kwake, utazalisha megawati 2115 za umeme ingawa kwa sasa Tanzania inazalisha megawati 3,404.
View attachment 3221038
Soma: Kamati ya Bunge: Bwawa la Nyerere litakamilika Juni 2024, Tsh. Trilioni 5.85 zimelipwa tayari
Tumechoka na hizo hadithi
 
Ikikamilika mitambo yote, mkumbuke kushusha sasa bei ya umeme ili wananchi nao waondokane na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa, na ambayo inachangia uharibifu wa mazingira.

Wenzetu wa nchi zilizoendelea, kila kiti wanategemea umeme! Sisi huku kwetu umeme unaonekana kama ni anasa! I think you can do it. Na ile gesi yetu ya Mtwara nayo ikiwezekana muanze kuisambaza kwenye magari, na majumba ya wananchi ili maisha yao yawe mepesi.
 
Mama anafanya kazi polepole sana.angekuwepo mzee magu angekuwa ameshamaliza kitambo huo mradi
 
Back
Top Bottom