SoC02 Mitandao ya kijamii ni fursa au ni mzigo kwa vijana wa kitanzania?

SoC02 Mitandao ya kijamii ni fursa au ni mzigo kwa vijana wa kitanzania?

Stories of Change - 2022 Competition

masai96

Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
7
Reaction score
5
1.0 Utangulizi
1.1 Mitandao ya kijamii imekua ni sehemu inayo wakutanisha watu kutoka pande mbalimbali za dunia, mitandao hii imeiminya dunia na kifanya ndogo kama kijiji kimoja. Kile kijiji ambacho taarifa husambaa mithili ya upepo wa kipupwe na kumfikia kila mwenye hamu ya kusikia.

Mitandao hii imekua na faida nyingi kwa wale wenye busara na akili ya namna ya kuitumia lakini pia imekua na hasara lukuki kwa wale waliobaki kuwa walimbukeni wasioona fursa penye fursa.

Swali la kujiuliza ni je sisi vijana wa kitanazania tupo kwenye kundi gani? Je tumebaki kuwa walimbukeni wa kuwafaidisha na kuwapa mkate wale waliofungua macho yao na kuuona mkate au na sisi tumekua miongoni mwa wavunaji? Makala hii ina lengo la kuwafikirisha watumiaji wa mitandao haswa vijana wa kitanzania waweze kufikiri na kufumbua macho yao ili waweze kujinufaisha na fursa zinazopatikana kwenye mitandao ya kijamimii ambayo imekuai kitugharimu mamilioni ya fedha za bando, muda pamoja na kuturaibu bila ya faida yeyote.

2.0 Fursa zipatikanazo kwenye mitanzao ya kijamii
Nimepita kwenye mtandao wa Smart Insights ukaniambia kwamba watu bilioni 4.70 ambayo ni sawa na ailimia 59 ya watu wote duniani wanatumia mitandao ya kijamii, ambapo mabilion ya fedha zimekua zikitumiwa kuingia kwenye mitandao hiyo huku pia mabilioni yakiwa yanaingizwa na watu kwenye mitandao hiyo.

Kwenye shughuli yoyote ya kiuchumi, moja kati ya rasilimali muhimu ni rasilimali watu hivyo kwa wingi wa watu wanaotumia mitandao ya kijamii inamaanisha upatikanaji wa nyenzo muhimu katika biashara na uchumi.

Hivi sasa sio lazima uwe na jengo la duka ili uweze kuuza bidhaa zako, vilevile sio lazima ukusanye watu kwenye ukumbi ndipo uweze kuwaburudisha, sio lazima pia kuwakusanya watu kwenye darasa moja ili uweze kuwapa maarifa mbalimbali (kuwafundisha), haina ulazima pia kupeleka tangazo lako redioni au kwenye televisheni ili liwafikie walengwa kinacho hitajika ni wewe kuwa na simu janja na salio (bando) pamoja na kuwa mbunifu, hapo lengo lako litakua limetimia.

Njia ya kutumia mitandao ya kijamii kufanya biashara mbalimbali imekua ni ya kawaida katika miaka ya karibuni. Biashara na miradi mbalimbali kama vile matangazo ya biashara, maduka ya kuuza bidhaa mitandaoni, kutoa mafunzo mbalimbali, kuburudisha na biashara nyingine nyingi.
Kulingana TCRA (2017) watanzania milioni 23 wanatumia internet hii ni sawa na asilimia 45 ya watanzania wote na idadi hii imekua ikiongezeka maradufu.

Wakati nchi zingine haswa nchi zilizo endelea zikitumia mitandao ya kijamii kama njia ya kujipatia ajira, watu wengi kwenye nchi masikini (Tanzania ikiwepo) wamekua wakitumia mitandao hii bila ya manufaa yeyote. Hii inapelekea idadi yetu kuonekana katika namba tu bila kuonyesha ushindani au kuleta changamoto zozote.

3.0 Je sisi vijana wa kitanzania ni mkate ulio mezani kwaajili ya walaji au nasisi ni miongoni mwa walaji mezani (are we the food to be consumed on the dinner table or we are among the consumers on the dinner table)?.

Katika miaka hii ya utandawazi imekua ni kawaida kwa nchi zilizoendelea kugombania bara la Afrika kutokana na fursa ya rasilimali watu inayopatikana katika bara hili, nchi zilizoendelea zimekua zikiiona bara la Afrika kama chakula kilichowiva tayari kwa kuliwa, hii inamaanisha kuwa katika bara la Afrika kuna soko la bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa katika nchi zilizo endelea.

Hii haiishii tu kwenye kugombaniwa kama soko la bidhaa zinazo ingizwa nchini mwetu bali hii inaenda mbali hadi kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wa waafrika tumebaki kuwa watumiaji wa mitandao hiyo bila ya kujipatia faida yeyote na bila kutumia fursa zinazopatikana humo.

Wakati wenzetu wakikaa mkao wa kula kwa kubuni namna ya kuvuna mitanzao ya kijamii, sisi tumeendelea kubaki kama wavunwaji, tumeendelea kuongeza idadi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao badala ya kutufaidisha, imekua uraibu kwetu.

Vijana wa kitanzania na waafrika kwa ujumla tumebaki kutengeneza fursa kwaajili ya watu wengine bila ya sisi kuziona fursa hizo ilhali sisi ndio wahitaji wakubwa wa fursa kuliko hao tunao watengenezea fursa. (We turned to be a food on the dinners table to be eaten instead of being among of the eaters).

Unaweza kukuta kijana wa kitanzania yupo tayari kununua bando kwaajili ya kuingia mtandaoni kupata umbea lakini huku hana uhakika wa hata hela ya kula, yaani mtu yupo tayari kulipia gharama ya kupata umbea kwenye Mange Kimambi App, ilhali lunch yake ni ya kubahatika. Huu ni uraibu wa kupindukia.

Sisemi watu wasiingie mitandaoni kupata habari na kuburudika lah hash! Sisemi pia watu wasitafute umbea mitandaoni lah hasha! Ninachosema ni kuwa tujaribu kuona fursa kwenye mitandao ya kijamii, kama wewe unalipia kupata umbea kwenye Mange kimambi App basi uwe unajua namna ya kupata faida kupitia umbea huwo.

Tusibaki kuwa watumwa kwa hiari yetu, tufumbue macho yetu tuone mwanga, mwanga utupao uhuru wa kifikra na kimali, mwanga utakao tunufaisha, tusibaki kuwa wasindikizaji bali nasisi tuwe washindani, nasisi tuwe ni miongoni wa wanaopeleka mkono mezani kujipatia mlo.

Tutumie mitandao kwa manufaa yetu na tusibaki kama watumiaji wa mwisho tu bali na sisi tubuni vitu ambayo watu wengine wanaweza kuvitumia.

Mitandao ina nguvu, ina ushawishi, tusibaki kuwa washawishiwa tu bali nasisi tuwe ni miongoni mwa washawishi, tuwe miongoni mwa wavunaji shambani, wavuvi baharini, na wachimbaji migodini.

4.0 Je Vijana wa kitanzania Tujue nini na tufanye nini?
Kwanza kabisa, tufahamu kuwa mitandao inafaida nyingi ambazo huambatana na hasara pia, hivyo basi umakini unahitajika katika kuitumia, kama ilivyo kwa dawa za kutibia ukiizidisha huleta madhara makubwa mwilini lakini ukitumia kwa kiasi kama inavyoelekezwa basi hutibu na kuponya. Hivyo na sisi tuwe watumiaji wa kiasi tusizidishe.

Pili, utumiaji wetu uwe wa manufaa, tusikubali kutumia mitandao kwa kujifurahisha tu bali tuwe tuna maswali (uncomfortable question) kuhusu faida ya kutumia mitandao.

Tatu, tujue kuwa matumizi ya mitandao kupita kiasi huleta uraibu, kwa wale ambao tumeshapata uraibu wa mitandao tutafute usaidizi wa namna ya kujitoa kweny uraibu huwo. Tutumie mitandao kwa kiasi na kwa manufaa.

NB: Makala hii haimaanishi kuwa watanzania wote wanatumia mitandao bila ya manufaa yeyote, kuna baadhi ya watu wa kupigiwa mfano katika kunufaika na matumizi ya mitandao laikini idadi ya wanufaikaji ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watumiaji wa mitandao.
 
Upvote 1
Hii nimeandika kutokana na kuwa nilimshuhudia rafik yangu...ananunua bando ili aangalie vtu ambavyo sio vya msingi hata kwenye mitandao ya kijamii....lakini baadae ananizima hela ajipatie mahitaji ya msingi kabisa...nilipo fanya utafiti nikagundua sio yeye pekee...bali wengi wetu tume be addicted na mitandao...mbaya zaid hatufanyii vtu vya msingi vya kutuingizia kipato
 
Back
Top Bottom