SoC02 Mitandao ya kijamii ni njia rasmi ya habari. Mashirika ya umma yarasimishe hii njia yenye ufanisi zaidi kwa sasa

SoC02 Mitandao ya kijamii ni njia rasmi ya habari. Mashirika ya umma yarasimishe hii njia yenye ufanisi zaidi kwa sasa

Stories of Change - 2022 Competition

Des Noel

Member
Joined
Aug 8, 2022
Posts
5
Reaction score
12
Umeme ukikatika tunasubiri kwa dakika 5 tu labda utarudi sababu ni kawaida ya nchi yetu, na baada ya dakika 5 umeme haujawaka, tunajaribu kutafuta taarifa kama shirika la umeme lilitoa tangazo juu ya umeme kukutika leo.

Unaitafuta TANESCO ubungo katika mitandao ya kijamii, ila inakuja tanseco account ya tanzania nzima na admins hajibu comment za watu.

Unajaribu kupiga simu , unaangalia namba imeandikwa huduma kwa wateja mwanza,tabora, shinyanga, unajiuliza kama tatizo limetokea tu mtaani kwangu hivi itawezekana kwa mtu anae deal na eneo kubwa kama hili kutatua tatizo langu la hapa mtaani kwangu? kitu kizuri simu haijapokelewa.

Nikaamua tu nisubiri mpaka watakapo uwasha umeme wakioenda wenyewe.

Siku nyengine maji bombani hakuna, siku ya kwanza, ya pili mpaka wiki inapita taarifa rasmi hakuna, mitandao yao ya kijamii hakuna update zaidi ya mwezi umepita, unaishiwa nguvu na raha ya nchi yako mwenyewe.

Umeme unakatika bila taarifa rasmi mara kwa mara ila hizo taarifa endelezi tunazitoa wapi ili wanachi warizike?

Pendekezo langu

Mashirika ya umma yawe na account za mitandao ya kijamii ya kiwilaya

Na yenye kutoa taarifa muendelezo kwa kila siku kwa mfano" umeme au maji umekatika leo katika kijiji fulani na hilo tatizo limeathiri eneo hilo tu na mafundi wanashughulikia"

Admins wawe na muingiliano mzuri na watu kwa kutoa mrejesho na kuchukua maoni na kuyafikisha sehemu sahihi kwa uharaka wake

Huduma kwa wateja mawasiliano yawe ya kiwilaya.

Kuzima umeme au maji kutopatikana kunakekera sana ila inakera zaidi bila kujua wapi utapata taarifa rasmi na kwa wakati

Mashirika ya umma yanapaswa kurasimisha mitandao ya kijamii
 
Upvote 0
Back
Top Bottom