KERO Mitandao ya Mawasiliano kukata pesa ya salio bila ridhaa wala taarifa

KERO Mitandao ya Mawasiliano kukata pesa ya salio bila ridhaa wala taarifa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Mar 20, 2024
Posts
8
Reaction score
0
Habarini wanajukwaa,

Jamani naomba kufahamu kuhusu hii mitandao ya smu. Nimekuwa nikiweka Salio katika mtandao X mfululizo,
jana asubuhi nimeweka salio kwa rusha nikaunga vizuri, jioni wakati narudi mishe nikapitia kwa wakala nikaweka Salio, nafika nyumbani niunge salio naambiwa halitoshi wamekata 199/=Tzs

Nikapiga huduma kwa wateja mara mbili tofauti na majibu yao yalikuwa ya kupishana

1. Alijibu nimejiunga na huduma ya mdundo music (hivi karibuni) ambayo muhusika anakuja na uwezo wa kupakua nyimbo za kiafrika. Nikahoji maswali je, kupitia kompyuta zake anaona taarifa zinasema nimejiunga lini? Anasema hazionekani taarifa hizo.

Swali kwa mtandao X
Wanasema hiyo PESA wanakata kila siku kama gharama ya huduma uongezapo Salio;
1. Je, kama nimejiunga hivi karibuni na sio leo kwanini siku zote za nyuma walikuwa hawakati na wanajua nimejiunga na hiyo huduma?

2. Asubuhi nikiweka salio kama nikua nimejiunga na huduma kwanini wasikate salio la kwanza kuwekwa kwa siku hiyo ya Jana wakate jioni? Au ukiweka Salio ukaliacha bila kuunga kifurushi kwa zaidi ya nusu saa wanajilipa Salio lako kwa maamuzi Yao?

3. Wanawezaje kumjibu mteja umejiunga (hivi karibuni) hivi neno karibuni linamaanisha nini kwamba hana rekodi sahihi ya lini mteja alijiunga na huduma au wanaguess tu kwamba ulijiunga na huduma?

4. Kwa Sheria za TCRA zinasemaje /TRA meseji ya malipo ya huduma yoyote si ndo risiti ya mteja kama manunuzi ya salio, huduma, muamala, bills kwanini wakikata hela wanazosema umejiunga huduma hawarudishi meseji ya kuthibitisha umekatwa fedha Fulani? Mbona huduma nyingine wanatumia meseji?

5. Wanasema unaweza ukajiunga kwa kujua au kutokujua? Hawajanilezea huduma hii inamfikiaje mteja mpaka anajiunga bila kujua wao wanasema kupitia link na laini hii haikua kwa simu kubwa. Je, nawezaje bonyeza link kwa simu ndogo (kiswaswadu) na nikawa eligible kuwa subscribed?

Na kama wanatumia meseji za link ya kujiunga au ni kwa kubonyeza namba kujiunga? Kwanini hawatumi meseji za mrejesho wa makato hayo?

Hawa jamaa wanatuibia, wamekata salio nikiwa na jambo la muhimu sana kulifanya siku ya Jana, imenisababishia kukwama baadhi ya mishe zangu maana sikuwa na uwezo wa kuitafuta vocha tena iliko.

Hawa watu tunawashtaki vipi?

Pia soma > KERO - Hakuna usalama kuacha salio kwenye simu
 
Back
Top Bottom