Mitandao ya simu imekumbwa na nini hivi karibuni?

Mitandao ya simu imekumbwa na nini hivi karibuni?

Good Father

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
10,321
Reaction score
18,574
Wakuu habari za leo.

Sijui wenzangu huko simu zenu vipi lakini siku za karibuni napata shida sana kutumia huduma za Tigo pesa na Mpesa mara kwa mara huduma haipatikani hasa jioni.

Hali hii zamani haikuwepo serious kiasi hiki ikilinganishwa na sasa.

Lakini hali ilivyo sioni wala kusikia wahusika wakitoa taarifa kwa wateja kuhusu hali hii.

Kuna muda unaweza kulala njaa na una pesa kwenye simu, sio tigo sio voda, sijui watumiaji wa mitandao mingine kama airtel na halotel wanapitia haya?
 
Siku hizi ni kama shida imekuwa kubwa zaidi hasa siku za weekend kuanzia Ijumaa. Siyo data, siyo voice, siyo apps, hali imekuwa tabu sana. Ni kama hakuna hata mtu anayejali kama kuna tatizo maana sijawahi kuwasikia TCRA wakitolea ufafanuzi wowote wa shida zinazowapata watanzania kutpitia huduma zisizoridhisha za mitandao ya simu pamoja na kuwepo malalamiko mengi ya wananchi. Kwa level ya technolojia iliyofikiwa sasa duniani, ni aibu wananchi wa TZ kuendelea kulalamikia huduma mbovu za mitandao ya simu. Umefika wakati sasa wa kuhamia kwenye sattelite kwa ajili ya mawasiliano kupitia kama 'star link'. Nchi iangalie uwezekano wa kuwekeza upande huo wa technolojia ili wananchi waendelee kupata huduma rahisi na za uhakika za mawasiliano.
 
Back
Top Bottom