Mitandao ya simu iongeze umakini katika maombi ya ku recover password

Mitandao ya simu iongeze umakini katika maombi ya ku recover password

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Nimeona malalamiko ya Wadau wakilalamika password zao zilibadilishwa muda mchache baada ya kuibiwa simu zao na fedha kutolewa kwenye account. Huenda mitandao ya simu hukubali maombi ya kubadilisha password kwa namna dhaifu na matapeli kutumia mwanya huo kuomba kubadilishiwa password na kuweza kumuibia mtu.

Kwa uchunguzi nilioufanya , wateja kadhaa wamedhibitisha kubadilishiwa password zao kwa haraka bila kuulizwa taarifa za msingi ambazo zingebainisha Kama wao niwamiliki wa lain husika.

Pia wengi hudai taarifa za nida Kama , Majina kamili na tarehe, mwezi wa kuzaliwa huulizwa, kimsingi taarifa za nida hupatikana kirahisi na haitoshi kubaini mmliki wa simu kadi ama laa

Mambo wanatoweza kufanya ili kuimarisha Usalama wa watumiaji wao
1. Kutokukubali kwa haraka maombi ya kubadili nywila walau masaa 24 baada ya kutuma maombi.

2. Mteja kutakuwa kuwasiliana taarifa zake katika Shop ya kampuni husika au tawi lolote lililokaribu naye.

3. Customer care waelekezwe namna ya kuwabaini matapeli pale wanapoimba kubadilishiwa password, kwamfano Kama Kuna mtu amesahau password bila Shaka nilazima akumbuke namba mojawapo , au taarifa nyingine za miamala.

4. Kurahisisha mawasiliano ya huduma kwa wateja ili kutoa Taarifa za upotevu wa laini . Kwasasa ukitaka kuwasiliana na mtandao fulani hasa Vodacom utakesha mpaka umehudumiwa waweke namba maalumu yabkupiga kurepot kupotewa na lain au simu ili iwe rahisi kufungua.

5. Finger print itumike
Mwisho Wadau mnaweza kuongeza
 
The best way apo ni fingerprint authentication tu wakati wa ilo zoezi la kubadilisha hio Nywila ndio matapeli watakimbia kusema Sijui Customer care wapewe more seminars hio haita work out Kwasababu at some circumstances they are part of the plan
 
Nikweli kaka
 
Sasa hizo shop ndio wezi wenyewe. Wana renew, pesa inarudi halafu wanafanya PIN RESET.
 
2. Mteja kutakuwa kuwasiliana taarifa zake katika Shop ya kampuni husika au tawi lolote lililokaribu Naye
Tunaoishi kijijini tutateseka sana.

La msingi kila mteja laini yake ya muhimu aweke Sim Card lock. Na aepuke application za Mpesa, TigoPesa etc. Sababu sometime zinaruhusu login kirahisi.

Naungana nawe Pin reset ifanyike kwa fingerprint.
 
🙏🙏
 
Back
Top Bottom