Sungurawembe
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 414
- 55
Habari wana-JF
Ni leo nimekutana na binti mmoja akilia kuingizwa mjini na wajanja,Kwani yeye anafanya kazi katika vibanda vya huduma ya pesa kama M-pesa,TigoPesa n.k
Mambo yalikuwa hivi, alipokea sms kutoka kwa boss (fake) wake ikimwambia mtumie pesa laki tatu mwenye namba 0713xxxxxx na kama flot haitoshi mwambie una kiasi gani, asimpigie simu yupo kikaoni na afanye haraka kwani zinahitajika hizo pesa.
Bila ajizi baada ya kuona kweli ni namba ya boss wake hakutaka kuhoji chochote na kutuma Tsh 180,000 kwa huyo mudukuzi wa mitandao na huyo bosi wake amekana kwa kusema hakumtaka kufanya hivyo.
sasa ni jambo la kujiuliza vipi huyo mtu aliingilia mawasiliano yao au wafanyakazi wa Tigo wameuza habari hiyo? au ni boss wake anataka kufukuza kazi kijanja huyo binti kwani na yeye ni mwanamke!
Tafadhalini ushauri wenu kwa huyo binti