Mitandao ya simu si salama

Sungurawembe

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
414
Reaction score
55
Habari wana-JF
Ni leo nimekutana na binti mmoja akilia kuingizwa mjini na wajanja,Kwani yeye anafanya kazi katika vibanda vya huduma ya pesa kama M-pesa,TigoPesa n.k

Mambo yalikuwa hivi, alipokea sms kutoka kwa boss (fake) wake ikimwambia mtumie pesa laki tatu mwenye namba 0713xxxxxx na kama flot haitoshi mwambie una kiasi gani, asimpigie simu yupo kikaoni na afanye haraka kwani zinahitajika hizo pesa.

Bila ajizi baada ya kuona kweli ni namba ya boss wake hakutaka kuhoji chochote na kutuma Tsh 180,000 kwa huyo mudukuzi wa mitandao na huyo bosi wake amekana kwa kusema hakumtaka kufanya hivyo.

sasa ni jambo la kujiuliza vipi huyo mtu aliingilia mawasiliano yao au wafanyakazi wa Tigo wameuza habari hiyo? au ni boss wake anataka kufukuza kazi kijanja huyo binti kwani na yeye ni mwanamke!

Tafadhalini ushauri wenu kwa huyo binti
 
Mbona huo wizi wa kawaida na unaenda kuexpire kama Mimi naye muajili lazima nimpe semina.
 
Hiyo kawaida sana, siku hizi angalau wameacha huo utapeli ila wengi tushaingiaga mkenge wa aina hiyo.
 
Siku nyingine asitume mpaka aongee naye kwenye simu..utapeli wa aina hii ushakuwa kawaida sasa hivi
 
Kuna uzi kama huu uliwahi kuletwa.

Ukweli hili hufanywa na wataalam wa IT wa Kampuni Husikaa.

Wizi huu ni sawa na issues za Bank Tellers na kuhusishwa na Majambazi
 
Upo mwingine unapigiwa sim na jamaa anajifanya castamer care anakutisha til yako inakariba ku expare chukua empty unisomee namba nikusajirie, unasoma mara jamaa anakutajia namba kuwa ndo uliyo sajiriwa anakwambia hamishia pesa yako yote ktk no hiyo halaka kabla hazijafia humo, kumbe no ni yake, mweee jamaa anasogelea nyama choma na supu ya mbuzi. pia ka bia ka baridi
 

Hahaha, hapo kwenye nyama choma bhana, umeongea kwa hisia sana mkuu haha
 
Siyo kwa Boss tu, hata kwa mtu wa kawaida, usimtumie pesa yoyote mpaka uongee nae kwenye simu na uthibitishe. Ni kheri ukae kimya uje ulaumiwe baadae kama ilikuwa ni kweli, kuliko kutuma alafu ukaja kufedheheka kwa kutapeliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…