Uchaguzi 2020 Mitano aliyotawala Rais Magufuli inamtosha, arudi Chato apumzike

Uchaguzi 2020 Mitano aliyotawala Rais Magufuli inamtosha, arudi Chato apumzike

mcoloo

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
918
Reaction score
1,402
Yapo aliyoyafanya ambayo ukitizama kwa juu juu utadhani kuwa Yana manufaa kwa watanzania lakini kwa msingi wake ndo yamechangia kudidimiza maisha ya wananchi.

1: Utitiri wa Kodi kwa mtizamo wa haraka haraka utaona kuwa Ni Jambo jema serkali inakusanya mapato kwa wingi,lkn kinyume chake hiyo Kodi isiyo kuwa rafiki na wafanya biashara imefanya wafanya biashara kujikuta hawapati faida kwenye biashara na matokeo yake biashara zimekufa.

2: Ununzi wa ndege si jambo Baya ila lilifanyika kwa mihemuko na kutafuta sifa, hivyo kupelekea fedha nyingi kuelekezwa huko, na matokeo yake hizo ndege hazija rejesha hata 1/3 ya fedha zilizo tumika. Na ndio maana hatuja sikia Tambo, zozte zinazo husu ndege. Kwani hata ukaguzi wa CAG hakubaliwi kugusa eneo hilo.

3: Kuwekeza katika miradi mikubwa sio dhambi ila miradi hii ulitakiwa kuioatia vipaumbele kuliko ilivyo fanyika kwa papara na mihemuko , matokeo yake ni kwamba fedha zimeelekezwa huko na kusababisha mzunguko wa fedha kwa wananchi kuwa mdogo hivyo kudidimiza uchumi wa mtu mmoja mmoja.

4: Serikali ilipambana na wawekezaji katika sekta ya madini matokeo yake ni kupata hasara, na kinacho dhihirisha ni ukimya wa Hali ya juu kuhusu hiyo sekta nk.

Maendeleo ya msingi kabisa huanza na kuboresha maisha ya watu katika nyanja zote.

Na ndio maana kama tutafanya kosa la kumrudisha huyu asiye shaurika, mwenye kujiona kuwa ana akili kuzidi watanzania wote, mwenye kupenda sifa na asiye na huruma kwa wananchi na hili utalipima wakati wa majanga huwa hayuko karibu na wananchi, mtu ambaye hata kushiriki kwake kwenye misiba ilikuwa shida Hadi alipo semwa semwa Sana. Tuta ukaribisha umaskini ambao kuja kuurekebisha utachukua zaidi hata ya nusu karne zijazo.

Huyu miaka mitano hii aliyo waingiza watanzania kwenye umaskini mkubwa hivi inamtosha. Akapumzike Chato.
 
Naungahoja mkuu, ili tumuachia yule jamaaa mshudia miujiza ya yesu, ilikuomba huruma ya Watanzania wampe uraisi kwa lazima kama kifuta machoziii. Huku akijawa kiburi, dharau, fedhuri na matusi mengi mdomoni.

Akijaribu kusoma Sera yuko empty kabisa kichwani, kiasi ambacho hata chama chake wanajuta kumpa ridhaa ya kupeperusha bendera yao kuomba uraisi.
 
JIKONO JANDAMA ni Mkemia hana ufahamu wowote wa uchumi halafu anafanya kazi kibabe bila ku_consult wataalam na matokeo yake ndio hayo uliyoyataja. Lazima apumzishwe.
 
Naungahoja mkuuuu, ili tumuachia yule jamaaa mshudia miujiza ya yesu, ilikuomba huruma ya watanzania wampe uraisi kwa razima kama kifuta machoziii. Huku akijawa kiburi, dharau, fedhuri na matusi mengi mdomonii.

Akijaribu kusoma Sera yuko empty kabisa kichwani, kiasi ambacho ata chama chake wanajuta kumpa ridhaaa ya kupeperusha bendera yao kuomba uraisi.
Kwani Hawakupanga njama za kumuua, mnyonge mnyongeni lkn hakii yake mpatieni. Lisu ana uoeo mkubwa kuliko mtu yeyote ndani ya CCM, ukibisha mtaje yeyote yule ili tukupe madhaifu yake.

Vipi bana nawe unakuwa Kama Wabunge wa CCM kila kitu kwao Ni ndiyoooooo, ndiyoooooo.
 
Si mlikuwa mnataka Rais dikteta, mara hii Mmeshamchoka?

Kaeni mkijua madikteta huwa hawaondoki madarakani kirahis rahisi.
 
Kwani Hawakupanga njama za kumuua, mnyonge mnyongeni lkn hakii yake mpatieni. Lisu ana uoeo mkubwa kuliko mtu yeyote ndani ya CCM, ukibisha mtaje yeyote yule ili tukupe madhaifu yake.

Vipi bana nawe unakuwa Kama Wabunge wa CCM kila kitu kwao Ni ndiyoooooo, ndiyoooooo.
Kama walipanga kumuua hao CCM, kwanini hamjawapeleka mahakamaniii!?

Ushaidi mnao kwamba waliopanga kumuua mwali wenu ni hao CCM, kwanini hajaenda ata kuripoti mahakamani?

Huyo jamaaa yenu simwanasheria mahiri saanaa, mbona hafunguikesi za kuwashitaki mahakamani hao CCM kamakweli anaushaidi wao ndio waliomshambulia?

Anakwama wapi shujaaa wenu?
 
Watanzania tumeshuhudia maiti za watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba.

Watanzania, tumeshuhudia wenzetu wakitekwa na kupotezwa, wafanyabiashra wakifilisiwa.

Tumeona ndugu na jamaa zetu wakifunguliwa makesi makubwa na yasiyo na dhamana.

Huyu mtu hatufai kabisa.
 
Achukue madege yake akayapaki chato apige nayo picha.
 
Kwani Hawakupanga njama za kumuua, mnyonge mnyongeni lkn hakii yake mpatieni. Lisu ana uoeo mkubwa kuliko mtu yeyote ndani ya CCM, ukibisha mtaje yeyote yule ili tukupe madhaifu yake.
Vipi bana nawe unakuwa Kama Wabunge wa CCM kila kitu kwao Ni ndiyoooooo, ndiyoooooo.
chadema nzima mwenye akili ni mbowe pekee na sio huyo mpyayukaji asiejielewa, kwanza watanzania washamtoa thamani baada ya kuonesha unafiki kwenye sakata la madini.
 
Sasa hivi wanataka kuwarasimisha waganga wa kienyeji/ witch doctors. Watumishi wa Mungu wanachekelea tu
 
Aliyekuwa na akili timamu hawezi kumpa kura huyo yesu feki! Aje huku Chato aendeleze kuvua furu.
 
Naungahoja mkuuuu, ili tumuachia yule jamaaa mshudia miujiza ya yesu, ilikuomba huruma ya watanzania wampe uraisi kwa razima kama kifuta machoziii. Huku akijawa kiburi, dharau, fedhuri na matusi mengi mdomoniii.
Akijaribu kusoma Sera yuko empty kabisa kichwani, kiasi ambacho ata chama chake wanajuta kumpa ridhaaa ya kupeperusha bendera yao kuomba uraisi.
Mkuu waweza sema ni tusi gani amekutukana au kumtukana mtu? Naomba unifahamishe tafadhali
 
Kama walipanga kumuua hao CCM, kwanini hamjawapeleka mahakamaniii!?
Ushaidi mnao kwamba waliopanga kumuua mwali wenu ni hao ccm, kwanini hajaenda ata kuripoti mahakamani?
Huyo jamaaa yenu simwanasheria mahiri saanaa, mbona hafunguikesi za kuwashitaki mahakamani hao ccm kamakweli anaushaidi wao ndio waliomshambulia?
Anakwama wapi shujaaa wenu??
Absence of evidence is not .......?
Kama uko timamu utakuwa umeelewa labda kama watoka pande zile.
 
Mkuu umeongea vema,kama kwa miaka mitano kashindwa kuajiri vijana wanaohitimu vyuoni sekta za muhimu kama elimu na afya,ajira zisizo rasmi ndo 0 kabisa,halafu apewe mingine ili aendelee na mipango yake ya kununua ndege.yeye anaona ndege in bora kuliko ajira za vijana,vijana tumkatae
 
Sera mbaya za uchumi mwanzo walituaniminisha kuWa watu wanaofungiwa biashara na wanao lalamikia ugumu wa maisha ni wapiga dili kweli njia muongo ni fupi,

Kitendo cha mwenyekiti wa CCM kuwa raisi kitaiondoa CCM mwaka huu , mgombe wenu kajipitisha bila kupingwa wakati auziki kwa wananchi kwasabu ya sera mbaya za uchumi

Nenda brela angalia garama za kusajili makampuni leo cost ziko juu sana ukilingani na miaka mitano iliyopita , Lseni za biashara pia ziko juu sana ukilinganisha na kipindi chanyuma kabla ya awamu hii mzunguko wa pesa sijui wameufanyaje zero ukulinganisha na 2015 .

Ukiachana biashara za ndani jaribu kuuliza mchakato wa exportion utazimia kodi kama zote kitu kidogo hadi sample zinatozwa kodi jiulize serekali wanatoza sample kodi huu kama sio umasiki wa kufiki nini jamani ??

Ukiwa na ndugu au rafiki nje ya nchi akakutumia simu moja au laptop moja utulipishwa ushuru, siku hizi kuna castom offices kwenye makamuni ya kubeba fivurushi kutoka nje ya nchi kama EMS DHL FEDEX nk.

Ukitaka kusafiri kwenda nje ya nchi longolongo uzushi mwingi sanaa Pasport za kusafiria kupitia uhamiaji nfano passport yangu inaisha 2025 kuna siku nilitaka kusafiri nikazuiwa wakaniambia passport yangu niyazamani nitafute mpya ebu imagine mamlaka imenipa pasport yenyewe kabla ya muda wa passport zetu kuisha wanazua watu bila sababu za msingi mamlaka hiyo hiyo ya uhamiji ndio watoaji wa hizo passport na ndio wazuaji wa watu kusafiri ubabaishaji wa kiwango cha juu sana awamu hii. Nikajalibu kufatilia mpya garama ni mala tatu ya passort ya zamani na ulasimu wakutosha yote haya ni awamu ya tano .

ANC kama Zuma angelikuwa mwenyekiti wao kama ilivyo hapa uchaguzi uliopita kingetumbuliwa kama ccm inyokwenda kutumbuliwa .
 
Back
Top Bottom