Ukifika hapa Mwenge jirani na Equity Bank na Mikocheni 'B' usawa wa Clouds Fm mitaro imejaa maji taka na taka.
Hii ni aibu ikiwa tunazo mamlaka za kuhakikisha usafi.
Wahusika DAWASA na Halmashauri Kinondoni tokeni maofisini mje mfiksi hizi kero, ni aibu kuwa na uchafu namna hii.
Inatakiwa wahakikishe wanakuwa na Cesspool Emptiers za kutosha na kubwa...ni aibu kwa mji kama Dar es salaam unaojipambanua kuwa wa kisasa kuwa na majitaka yanayotiririka tuDar sehem nying sana zilizo tambarare kuna shida ya sewage system.
haijaanza leo wala jana.
sewage system nying zimeziba na haikidhi uwezo wa kubeba taka nying.
Mfano baadhi ya maeneo ya Kawe, tandale, sinza. Pale mwenge kwa mama Ngoma ule mtaa unaitwa mtaa wa mavi. (Kila siku kuna haruf ya nya na maji machafu yanatoka juu ya ile sewage system).
Manispaa iangalie upya miundo mbinu ya maji taka waliyoiweka miaka 30 nyuma. haikidh mahitaj makubwa yaliyoko sasahiv.
cha ajabu Dawasa wanawawekea wateja wa maeneo hayo bill ya maji taka kila mwez kwenye bill za maji, hiyo hela inaenda wap? wakat miundo mbinu hawaboreshi.
ni uwajibikaji na kudhubutu. maana najua hela wanayo na inatosha .Inatakiwa wahakikishe wanakuwa na Cesspool Emptiers za kutosha na kubwa...ni aibu kwa mji kama Dar es salaam unaojipambanua kuwa wa kisasa kuwa na majitaka yanayotiririka tu