Miti kwa ajili ya kivuli

Mtimaji ama muarobaini ni fasta kabisa. Lakn ungepanda ya matunda ukapata faida mara mbili
 
kuna miti kama upo dar imepandwa pembezoni mwa barabara iendayo mwenge tokea Moroco ni mizuri sana kwa kivuli na inakuwa haraka- marawi yake yanakuwa kama ngazi ngazi hivi!
 
Ili usaidiwe inakubidi useme upo mkoa gani usijekuta upo Dodoma halafu ukaelekezwa miti ya DSM
 
Kuna mmoja naujua kwa jina la MDODOMA sijui jina lake la kitaalam ni mzuri na haunyauki hata kiangazi

driller⛏⚒
 

Zelkova tree nenda karibu na mlimani city ukiwa unatokea ubungo wanauza miti mizuri sana,

kwa faida zaidi panda mitiki pembeni ya nyumba yako
Dr. hiyo mitiki faida zake nini... ninapenda miti saana... nimeshazoea mitope tope miparachichi stafeli michungwa ambayo mwisho wa siku napata matunda.
 
Panda miembe mifupi mkuu. Au mikomamanga.

love thé love or hâte thé love.....
 
Dr. hiyo mitiki faida zake nini... ninapenda miti saana... nimeshazoea mitope tope miparachichi stafeli michungwa ambayo mwisho wa siku napata matunda.
Nafikiri mitiki ni mti ghali kuliko miti yote kwani ubao wake mkuu daby unatumika kutengeneza vitako vya bunduki na kutengenezea meli ni miti ambayo inafaida sana ukilima ekari moja unauuga umasikini.
Sehemu nyingi inastawi.......ila zaidi kwenye mvua za kutosha, joto la wastani na udongo wenye kina kirefu. Mashamba makubwa ya Teak yapo Tanga (Longuza), Morogoro (Turiani, Ifakara etc). Kazi kwako.....ukipata kijitabu cha mbegu cha Tanzania Tree Seed Agency kimeorodhesha maeneo kwa ufasaha zaidi.
Mimi binafsi nimeipanda kwangu na shambani japo si kwa wingi.
Mkuu ubao wa teak huwezi kuununua its very expensive na endapo ukilima hata ekari moja lazima mabenki waje wakubembeleze uwauzie.
 
Noted, nitautafuta... kwa Arusha naamini kama morogoro unastawi basi utastahimili
 
Hicho kitabu cha TTSA ninacho mkuu. Ila mitiki inachukua muda mrefu sana kufikia harvesting age about 25 years

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sasa mabenki yaje kukubembeleza kununua mbao/mitiki kwa ajili ya nini? Benki hazitengenezi furniture.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…