SoC04 Miti kwenye Wajenzi-Tanzania kwenye Vipengele vya kuijenga

SoC04 Miti kwenye Wajenzi-Tanzania kwenye Vipengele vya kuijenga

Tanzania Tuitakayo competition threads

Ntakasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2013
Posts
1,428
Reaction score
456
Kwenye miti hakuna wajenzi nadhani umesikia huu msemo mara kadhaa,Kwa tafsiri ya kimsingi ni kuwa, kuna namna saa zingine kunakuwa na nyenzo pasi uwezo.

Msemo huu hudhaniwa pia kuwa ni kitu kisichozuilika kama vile upele ambavyo haumpati mwenye kucha.

Lakini ikumbukwe kucha huota wakati mbadala unapotumika na tukirejea kwenye msemo wa kwanza –Wajenzi hujengwa palipo na miti.


AD_4nXferSi-N_OsAfJQc8mr3GD8XTFc8c6fgTKVschlkL6inSiKYAo7OLuSCjQxc2F9kf7rRoUm_2ANTS3BlaGyjSD9oO6e3wtN6vNbM5iyFO6ORUBvGi-0iVWwutShtzLBm5UNIIwhjYeydPTx3a1S17JFscG6




Tanzania yetu ni ya miti mingi na wajenzi wenye uwezo wa kujengwa ili kujenga na kuwa BORA na kuwa moja ya mataifa yanayohamasisha na kuchagiza maendeleo chanya barani na duniani.

Kuna miujiza ndani ya mipango elekezi yenye kulenga kurekebisha mifuko ya misingi ya maendeleo na kuleta Tanzania mpya.


ELIMU

Elimu ya Awali


Samaki mkunje angali mbichi, kama kuna sehemu ya kuanzia basi yamkini ELIMU ya awali ni eneo la kulikaribia na lenzi za uoni na kuhakikisha kuna mipango ya stadi za kuweza kumfanya mtoto awe mgunduzi na mwenye shauku ya kujua zaidi.

Mfano katika kila madarasa ya ELIMU ya awali (Miaka 3-6)

Kwanza iwe kwenye hesabu rasmi ya serikali na pia iwe na majaribio ya vitendo yanayohusisha teknolojia, ufundi na lugha katika maudhui ya umri wao mdogo unaohusisha mchezo na mafunzo


Elimu ya juu SANIFU

Eneo la pili kwenye ELIMU la kuzingatia ni uwanda mpana kwenye ELIMU ya ngazi ya juu lakini Ile ya kijamii

Kungepatikana vyuo vingi zaidi vya kijamii (community colleges) ambavyo vinashikana na stadi na kozi ambazo moja Kwa moja zinahusiana na jamii.

Veta ni sehemu ya mpango mzuri uliokuwepo lakini kuwe kuna machaguo ya wanafunzi wa kidato cha nne na cha SITA kuangalia wapi wanaweza kufanya vizuri zaidi na ili iwe ina muundo wa kufikika na wa kiuhalisia basi yamkini kila wilaya inastahili kuwa na chuo cha jamii husika.

Kwa mfano wilaya ya Temeke ikawa na ‘Temeke Community College’

ambapo kunakuwa zinatoka kozi za maeneo ya huduma zinazozunguka wilaya zote.

‘Bagamoyo Community College’ na wilaya nyinginezo


*Watoa huduma ya afya

*Watoa elimu wa shule za Awali

*Walinzi

*Wajasiriamali

*Wasanii



Sanaa


Hapa nikae kidogo, Sanaa ina nguvu mno na inaokoa jamii Kwa kujikita kwenye ubunifu na kuniweka Sawa kifikra na kimaendeleo.

Basi tukubali Kubwa wa nguvu yake inastahili Kubwa wa uwekezani wake ambapo ni dhahiri kila wilaya pia inastahili kituo cha utamaduni Kwa Kubwa wa kiserikali.

Mfano.

‘Ubungo Art Centre’

Iwe na eneo lake na mitaa yake ya kisanii yenye kuhusisha jamii kwenye mipango yake na kuwa kitivo cha wasanii wa wilaya yake.

Ni rahisa kuokoteza kila aina ya sanaa Kwa Mtindi huu kwenye ngazi ya kitaifa na kutoacha makundi mengine nyuma kwenye kuendeleza sekta hii


AD_4nXe5brgmFx_q9a9IclxEBxDHRs36W951dJrtAFGpITuvXoAipm4oTi0QEmOqa3Xm9lrG1UuXtAW80FPMsxOeburIM5rap--1FteW1M-2vpIpJlWljlM82Ge9whGipMslYXgET83FpAifFV_uBA321ntjVMNW


Orlando Towers ya Soweto | @afonography




Kwangu mambo haya matatu katika sekta ya Elimu ya Awali na ya juu-jamii inakusudia kuzalisha uthabiti katika sekta muhimu kama afya na hata kilimo, mambo ya kuzingatia kabisa, pia uzingatiaji wa sanaa na utamaduni buleta chachu ya mengi mazuri katika tasnia hii adhimu.

Nimeambatanisha sharing kutupia picha ya Tanzania tuitakayo.


TANZANIA TUITAKAYO


Ujumuishaji wa Awali

Watoto kutafuta majibu, kabla ya swali

Kupigia mstari

Ubunifu na utayari


Usomi wa kuchagua

Usomi wa kuamua

Usomi wa kutatua

Usomi wa kuzindua


Jamii kuzingatia

Jamii kuipalilia

Jamii kutolialià

Jamii kufanikiwa




Kipengele cha pili.


Siasa Safi



Nadhani hii inaweza kuwa ndoto lakini sababu sisi ndio wenye kuweza kubeba Maono basi Tanzania inaweza kubadilika mno kama tukiweza kuimarisha vyama vya kiraia vyenye malengo wa kuchangia mawazo.

Hapa sikai Sana maana kichwa kinagonga “dabo dabo”

Ila hii ni barabara yenye mwelekeo chanya.


Kodi zenye afya


Hakika tozo na kodi zisizo na tija ya kumuinua mwananchi mpambanaji hururudisha nyuma kimaendeleo.

Basi tutumie tu msemo huu

“Kwa yule ambaye vingi anapata, matarajio zaidi hutakiwa”

Kwa wafanyabiashara ambao wanapewa unafuu wa uendeshaji biashara basi yamkini inakuwa inaleta wepesi wa wao kurudisha kiasi cha kodi kinachotakiwa.

Ila kwa wapambanaji ambao huanza na mtajinwa nguvu basi wajengwe Kwanza na kuwezeshwa kukukua kwenye rasilimali za Mali ndio wasogezwe kwenye mfumo wa kuleta faida ya pesa ambayo huzaa Kodi.


•Vipengele vya kwanza ni vipengele vyangu vya Imani ya kubadilisha dira nzima ya maendeleo ndani ya miaka mitano hadi kumi na vinawezekana.


•Vipengele vya pili ni vile ambavyo vinategemea zaidi uongozi bora na demokrasia kuvifanikisha, basi tukiwa tunaweza nje ya boksi, tukumbuke pia kufanya maamuzi ya busara ya kuchagua viongozi wenye sera na sifa ya kuleta mabadiliko ya kweli.

Na ikibidi tuwe hao viongozi kwenye kila Nyanja tuiwezayo


Shukrani.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom