Miti mikubwa pines inauzwa

Miti mikubwa pines inauzwa

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Posts
5,329
Reaction score
5,024
Kuna mashamba matatu ya miti ya Mbao jamii ya pines ( pinus patulla), miti ina umri wa miaka 12 na 13. Miti hii iko kijiji cha Chogo Mufindi, ni 100km toka Mafinga kwa njia ya Ibwanzi, au 120km toka Iringa/Mafinga. Bei ya kila eka moja ni Tsh 1,200,000/. Mashamba yanafikika kirahisi.

Shamba la kwanza ni eka 5, lipo kando ya Barabara umri miaka 12, shamba la pili eka 50, miaka 13 gari linafika hadi shambani. Shamba la tatu eka 36, miaka 13. Barabara inaishia kama mita 400 hivi, pakisembuliwa gari linafika vizuri.

Wenye mashamba wapo dar, mmoja anauza ili aoteshe parachichi, wa pili anauza ili afanye mambo mengine na ku-replant eucalyptus.

Haya mashamba nayafahamu back ground yake vizuri sababu nilishiriki kuyanunua, kuotesha, kutunza na sasa kuuza. Karibuni.
 
Sipo mafinga kwa sasa, ila nakuja sana mafinga, na kiwanja changu kikubwa ni kwa babu kuku pale na Kalabash.
Sawa sawa mkuu! Kwasasa hivi tayari nilipata miti kifanya, Nikimaliza kazi nitakutafuta nije niicheki kama itakua haijauzwa.
 
Kuna mashamba matatu ya miti ya Mbao jamii ya pines ( pinus patulla), miti ina umri wa miaka 12 na 13. Miti hii iko kijiji cha Chogo Mufindi, ni 100km toka Mafinga kwa njia ya Ibwanzi, au 120km toka Iringa/Mafinga. Bei ya kila eka moja ni Tsh 1,200,000/. Mashamba yanafikika kirahisi.

Shamba la kwanza ni eka 5, lipo kando ya Barabara umri miaka 12, shamba la pili eka 50, miaka 13 gari linafika hadi shambani. Shamba la tatu eka 36, miaka 13. Barabara inaishia kama mita 400 hivi, pakisembuliwa gari linafika vizuri.

Wenye mashamba wapo dar, mmoja anauza ili aoteshe parachichi, wa pili anauza ili afanye mambo mengine na ku-replant eucalyptus.

Haya mashamba nayafahamu back ground yake vizuri sababu nilishiriki kuyanunua, kuotesha, kutunza na sasa kuuza. Karibuni.
Kijiji hicho nakijua, usafiri wake mgumu sana. Na mbaya sana ni msimu wa mvua
 
Ngoja mkuu Malila aje atuambie mti mmoja unatoa mbao ngapi za 2x2 labda,
Na bei ya shamba ni kias gani.

Nje ya hii biashara, kaka yangu Malila ni mtaalam wa sana wa haya mambo. Nilifanya nae biashara flan hivi miaka ya nyuma Kijiji kinaitwa "NYAVE"
Miti yote kwa asilimia kubwa inatoa 2x4 zaidi, 2x6 kidogo na ten hakuna, ila 2x2 unapata kama zote. Shamba la eka 36 na 50 yalicheleweshwa prunning na usafi.
 
Back
Top Bottom