Mitihani kusahihishwa upya

Ni kweli mitihani inarudiwa kusahiishwa naombeni nijulisheni

Ni Kitu kisichowezekana kisheria, mtihani unarudiwa kusahihishwa tu kama mtahiniwa amekataa rufaa na ametimiza vigezo hivyo ikiwepo kulipia na kujaza form(s)... otherwise maamuzi ya KISIASA yafanyike tu kwa UJINGA wakutaka kuwaridhisha wajinga wanaodhani WAMEFAULU wakati WAFELI...
 
Kwani ukirudiwa kwa sababu za kisiasa hayo MAZOMBI yatavaa viatu?
 
Umedanganywa kama na wewe ni sehemu ya hao Zombie, sahau sio kwa Tanzania, bajeti ya kazi kama hiyo haipo, na kama wakirudia itakuwa mbaya zaidi kwasababu wanaofundisha na wanaosahihisha ni hao hao ambao hawajaboreshewa mishahara, miundombinu ya kufanyia kazi, vifaa vya kufundishia (vitabu) na mengine mengi kinachopelekea wao kushindwa kufanya kazi ipasavyo wakati Waziri na watendaji wakuu wengine wakifaidi mihela na marupurupu kibao.
 
kazi ilifanyika vizuri ya usahihishaji hatuna wasiwasi na waliofanya kazi hiyo
hayo ndio matokeo kama mwanafunzi ana wasiwasi basi aende akakate rufaa
baraza ili asahihishiwe vinginevyo hakuna kitu wanafunzi wanaelewa walichofanya
hayo ndio matokeo yao.
 
kama serikali itarudia kusahihisha basi ifanye kwa matokeo kuanzia 2010. la sivyo ni upumbavu mtupu.
 
Gharama ya kulipia ada ya mtihani ni Tsh 35000/-x kwa idadi ya wanafunzi waliofeli
Serikali hii itapata wapi pesa ona Bunge la Bajeti
limesogezwa mwezi wa nne badala ya wa saba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…