Mitihani ya darasa la saba isitumike kama kigezo cha kwenda sekondari?

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Tanzania imeshauriwa kuwaruhusu watoto wanaomaliza darasa la saba kuendelea na masomo ya sekondari kwenye shule za serikali bila kuzingatia matokeo yao kwenye mitihani ya mwisho ya darasa la saba. Ushauri huo umetolewa na shirika la haki za binadamu la Marekani (Human Rights Watch) na Tanzania Child Rights Forums kwenye barua yao kwenda kwa Waziri wa Elimu.

Kwa sasa ili mwanafunzi aweze kuchaguliwa kwenda shule ya sekondari ya serikali ni lazima afaulu mitihani yake ya mwisho kwa kiwango kilichowekwa na serikali. Hata hivyo, mashirika hayo yanadai kuwa zaidi ya watoto 400,000 (sawa na aslimia 49.4) walifeli mitihani yao ya darasa la saba mwaka 2013.

Juliane Kippnberg wa Human Rights Watch anadai kuwa watoto wote wa Kitanzania lazima wapewe haki ya kuendelea na masomo ya sekondari kwenye shule za serikali bila kuzingatia matokeo yao kwenye mitihani ya darasa la saba. Anadai kuwa kutumia matokeo ya darasa la saba kama kigezo cha kuamua nani aendelee na masomo ya sekondari ni kinyume na haki ya mtoto ya kupata elimu.

Serikali inafikiria kuwa na sera mpya ya elimu ambapo itakuwa ni lazima kwa kila mtoto kupata elimu ya sekondari hadi kidato cha nne. Hata hivyo, sera hiyo mpya haigusii chochote kuhusiana na kutumia matokeo ya darasa la saba kama kigezo cha kuamua nani aendelee na masomo ya sekondari. Katika barua yao, wanadai kuwa mitihani ya darasa la saba itumike tuu kupima uwezo wa mwanafunzi lakini siyo kama kigezo cha nani aendelee na elimu ya sekondari.

Mashirika hayo yanapendekeza serikali iwe na sera mpya ya elimu na kuhakikisha kuwa mitihani ya darasa la saba isitumike kuzuia watoto kuendelea na elimu ya sekondari. Pia yamependekeza serikali iboreshe vitendea kazi kwenye shule za sekondari ili shule hizo ziweze kufundisha wanafunzi wengi.

Aidha mashirika hayo yanadai kuwa mitihani ya darasa la saba inachangia kukiukwa kwa haki nyingine za watoto. Kwa mfano, Human Rights Watch wanadai kuwa katika uchunguzi wao walioufanya mwaka jana walikuta kuwa watoto waliofeli mitihani ya darasa la saba walikuwa katika hatari ya kujihusisha kwenye machimbo madogo madogo ya madini.

Tanzania imetia saini Mkataba wa Kimataifa wa Haki ya Mtoto. Kwa mujibu wa mkataba huo, kila mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 ana haki ya kupata elimu. Je, tuache kutumia matokeo ya darasa la saba kama kigezo cha kuchagua nani aendelee na masomo ya sekondani na nani aishie kwenye elimu ya darasa la saba?

Barua hiyo kwenda kwa Waziri wa Elimu inapatikana: Letter by HRW and TCRF to Tanzania Minister of Education | Human Rights Watch

Invisible, gfsonwin, MTM, Kiranga, snowhite, Kongosho, Nyani Ngabu, Elly Andrew, xtra, TIQO, Enjoy Fumbo, MAKOLE, mwaJ, dedam, kyumana, mseveni, Masele Joe, kichwa kikubwa, buchuja, Chisco, Dr. Rama, Joseph Isaack, Meuzy, vanmedy, Issa Daudi, FALSETTO, Ramadhan vitalis, MDSON, chopeko, TAMBUA, Azizi Bin Adam, Chal, ndawo, Mdume, bshayo, Dark City, mgweno tajiri, Mkomawatu, ntamaholo, Baraka Roman, sundoka, Sam Love, swagazetu, ladyfurahia, Rugaijamu, Brother James, watu8, The Magnificent, Excel, Molembe, kbm, CHUAKACHARA, Sizinga, Munkari, BONGOLALA, Izack Mwanahapa, TUKUTUKU, Zogwale, kikokwe, Mhache, Njowepo, Mpita Njia, benzoo, Gama, Makupa, englibertm, Jabulani, Nivea, Window7, Mwl.RCT, mwekundu,
 
Kimsingi darasa la saba kuna kuchaguliwa zaidi ya kufaulu.

Kwa maana ya kwamba inabidi tusomeshe wale ambao tuna uwezo wa kuwasomesha, na hao wengine hatuwasomeshi si kwa sababu wamefeli, bali kwa sababu hatuna uwezo wa kusomesha wote.

Wazo la Universal Secondary Education linaweza kuwa zuri, lakini kama bado hata hiyo Universal Primary Education hatujaiweza tutakuwa tunafanya pupa kwenda kwenye Universal Secondary Education.

Na tunaweza kuingia katika mtego wa ku sacrifice quality for quantity.

Tumeshapata funzo katika zoezi la shule za kata.

Kama kuna mtu anapenda sana Watanzania wawe na Universal Secondary Education na serikali haina ubavu, basi aikatie fuba serikali.

The other question is, do we really need to give every right to everyone without condition?

Mtu anaweza kusema ana right ya movement kokote Tanzania na Tanzania ni nchi kubwa, hivyo ana right ya kuendesha gari azunguke, lakini bado atatakiwa kuona kwamba kuendesha gari ni privilege inayohitaji leseni.

Na kukosa kuendesha gari hakumnyimi kupanda basi na ku exercise right yake ya movement. Hizi basic right zinatakiwa ziwe basic in many senses, tusipoangalia tutasema kila mwananchi asiye na makazi Dar ana right ua kulala Ikulu, si State House na inaendeshwa kwa kodi ya umma?

What is education? Must education be provided by the government? Ukishajua (rather ukishapewa fursa ya kujua) kusoma na kuandika kwa nini serikali maskini ilazimike kukubeba hata kama hubebeki?

Kwa nini tusiangalie kwa mfano, kujenga a good library network, ku demistify mitihani kiasi hata mtu ambaye hajapata nafasi ya kusoma sekondari anaweza kujisomea na kufanya an O Level equivalent kama GED kwa Wamarekani? Mtu kama kweli anataka ku exercise his right to education mnampa library ile, vi coop vya elimu hivyo, path to private candidacy hiyo, anasoma na kupata an added layer of independence learning. Atakayefaulu hapo nyie mliofundishwa shule hamumpati ng'o.

Mimi naona kabla ya lofty and highfalutin goals, kwanza tuimarishe hiyo UPE watoto wamalize huku wana basic skills.

Otherwise utataka wote waende sekondari wakati robo hawajui kusoma na kuandika?
 
Hizi haki za binadamu hizi!

Mi naona zi puuzwe tu! Walianza mtoto wa kike ana haki ya kusoma!

Sahizi wanaanza kila mtoto ana haki ya kuendelea na sekondari!

Hili swala lipingwe tena kama ndoa za jinsia moja!
Watoto wanaoingia sekondari wapo ambao hawawezi hata kuandika neno JAMII FORUMS , afu wanataka na mat--ra wengine waliofeli la saba waendelee na sekondari!

Wanataka wakafanye nn sasa! Haya mashirika ya ulaya yasitupumbaze na haki zao za binadamu! Hebu tumalizane na suara la KATIBA kwanza !
 

Mi nataka mpaka chuo kikuu iwe bure kama Ujerumani, lakini huwezi kusomesha wote, utamaliza bajeti kwenye kujenga shule walimu utashindwa kuajiri.

Mambo yale yale ya shule za kata.

This ideal is an illusion that is good as a standard to be pursued ( sometimes these lofty goals are good for giving us a focus, as long as we remain realistic in our expectations), but it is not practical.
 
...Otherwise utataka wote waende sekondari wakati robo hawajui kusoma na kuandika?

Hata sasa hivi inadaiwa kuwa serikali inapika bomu la wasomi ambao hawatakuwa na manufaa kwa taifa, kwa sababu haiwezekani kuchagua mpaka mwanafunzi asiyekuwa na sifa ya kujiunga na kidato cha kwanza ili kujaza nafasi, wasomi hawa ndio wale wanaopasua watu vichwa badala ya miguu.

Baadhi wameelezewa kushangazwa kwao na Serikali kuchagua hata wanafunzi wenye ufaulu D kwenda sekondari. Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) alisema elimu ya Tanzania imekosa mwelekeo kutokana na mwaka huu Wizara ya Elimu kuchagua wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mpaka waliopata wastani wa alama ya asilimia 24 kwa kila somo, badala ya asilimia 44 ili kujaza nafasi katika shule za sekondari.

Nae Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikujombe (CCM) alisema haina maana kuona taifa linapeleka wanafunzi wengi sekondari wakati waliofaulu ni wachache. Mimi naona haina maana kujisifia kuwa tumefaulisha na kupeleka sekondari wanafunzi wengi wakati waliofaulu wachache, kama wamefaulu wanafunzi 100 tupeleke hao hao badala ya 200 ili kujaza shule," alisema Filikujombe.

Filikunjombe alipendekeza wanafunzi ambao wamepata wastani wa alama ya chini ya asilimia 70 kuachwa kabisa kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, badala ya kuwapeleka sekondari ili kwenda kujaza vyumba vya madarasa wakati hawana sifa ya kujiunga na elimu hiyo: Njombe, Iringa waponda matokeo darasa la saba - Kitaifa - mwananchi.co.tz

On the other hand, hawa wanaofeli tuwafanyeje? Obviously, hatuwezi kuchagua waliofeli kwa ajili tuu ya kujaza madarasa. One option ni kuimarisha elimu ya msingi ili kuongeza idadi ya wanaofaulu, but I can't seen this happening soon. Kuna mwandishi mmoja amehoji kuwa "leo mhitimu wa darasa la saba analazimika kuwa mchuuzi wa bidhaa lakini shuleni hakufundishwa chochote kuhusu namna ya kufanya biashara, ububifu wa biashara, namna ya kupata mtaji na masoko, kanunu za kufanya za kufanya biashara katika mazingira ya ushindani, ubunifu, kurhubutu, kutafiti masoko ndani na nje ya nchi, kufanya biashara kwa mtandao, namna ya kuongeza wigo wa mtaji, n.k." http://www.habarileo.co.tz/index.php/safu/18356-ujasiriamali-unawagharimu-wahitimu

Probably alikuwa anazungumzia suala zima la mtaala na suala zima la elimu ya ujasirimali. Could this be an option for the future?
 

.
Hiyo bure yaani ni ile ya kutolipia au kuwaacha tu waendelee mbele hata bila mchujo!

Na kama ni hivyo
Unakubaliana na kuwaacha hata wasiojua kusoma na kuandika! Nao wakajiite wanafunzi wa chuo kikuu?
 
.
Hiyo bure yaani ni ile ya kutolipia au kuwaacha tu waendelee mbele hata bila mchujo!

Na kama ni hivyo
Unakubaliana na kuwaacha hata wasiojua kusoma na kuandika! Nao wakajiite wanafunzi wa chuo kikuu?

Right hailipiwi mwana, ushalipia kupiga kura?

Wasiojua kusoma kuachiwa waendelee nishasema ni ujuha hapo juu.

Labda nimeandika lugha tofauti, nilichosema ni kwamba, hatuwezi kukimbilia kila mtu apate elimu ya sekondari wakati elimu ya sekondari inajengwa katika elimu ya msingi na elimu ya msingi hatujaiweza bado, watoto ndio hao wanamaliza darasa la saba hawajui hata kusoma Kiswahili.

Sasa hawa wasiojua kusoma Kiswahili ndio utaenda kuwafundisha kusoma "This is a Bunsen Burner" form one?

That is, if you have that Bunsen Burner at all!
 

And then some people have the nerve to wonder how did we end up with the likes of Mulugo!
 
Reactions: EMT
Mambo mengi ya Tanzania ni valuvalu sana, elimu ikiwa mojawapo.

Ni mwaka jana tu waziri wa elimu (au naibu wake kama sijakosea) alisema wale waliopata madaraja ya tatu na nne watapelekwa kwenda kusomea ualimu.

Akili gani sasa hizo? Mtu ambaye kashindwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya masomo yake ndo mnampeleka kwenda kusomea ualimu. Really?

Mambo mengine yanachosha kabisa hata kuyajadili maana ni ya kipuuzi kupita maelezo! Mtu unaweza kutadhani hao wanaofanya hayo maamuzi wana wadudu vichwani mwao.
 
mimi naunga mkono hoja ya HRW ,sema serikali itumie nafasi hiyo kama changamoto ya kuboresha elimu,nchi za wenzetu elimu ya ulazima ni hadi chuo kwanini sisi form four iwe issue kubwa?we have to move on now na serikali ijikita katika kuwekeza kwenye elimu
 
Kwa mfumo wa sasa wa Serikali na viongozi mbumbumbu na wasiojali hili suala hata likifanikiwa, bado itakuwa ni vigumu mno kutekelezeka kwa Tanzania, hizi ni baadhi ya sababu:

1. Shule nyingi za sekondari za Kijamii zipo mbali na makazi ya Wanafunzi na nyingine zimejengwa Porini hasa, jambo hili litamkatisha tamaa mwanafunzi kwani akishafikiria miaka minne ya mateso hataweza kuendelea.

2. Shule za sekondari ni chache mno ukilinganisha na idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba. Ikumbukwe kuwa, uchache wa wanafunzi wanaosoma sekondari sasa bado unakabiliwa na upungufu wa rasilimali fedha, watu na hata miundo mbinu haikidhi.

3. Utayari wa wanafunzi kupokea stadi mbalimbali kwa lugha ya kiingereza kwa masomo yote ya sekondari wakitokea huko msingi ni tatizo kwani kutakuwa na mhamo wa ruaza (paradigm shift) kwa kila kipengele kimhusucho mwanafunzi mmoja mmoja. kiakili, kimaumbile, saikolojia yake pia atakuwa hajakamilika.

4. maandalizi ya mwanafunzi shule za msingi ni hafifu, mfumo uliopo unalazimisha hata baadhi ya wanafunzi wanahitimu darasa la saba bila kujua KKK. (KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU) hili SI kosa la mwalimu, ni kosa la viongozi MBUMBUMBU wa serikali yetu. Mtaala wetu unamtaka mwanafunzi kuanzia chekechea awe na mkururu wa masomo. SAYANSI, AFYA, STADI ZA KAZI, KISWAHILI, KIINGEREZA, HESABU, Nk. Kwa mtoto wa kitanzania na wa kijijini hana utayari huyo. Zamani hadi darasa la pili mnasoma KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU TU. hayo mengine mnayakuta kuanzia darasa la Tatu. Ndio maana kulikuwa hata na mashindano ya Hati kikonyo. Leo hii hata hiyo hati kikonyo hakuna tena.

HATARI ILIYOPO....

Usije kushangaa hawa Mambumbumbu waliopo kwenye mfumo kwa sasa kwa barua hii wakaamua tu kwamba hakuna kufeli darasa la saba ila wanafunzi waende tu sekondari. Hawashindwi....

Hawatafanya mabadiliko makubwa kuanzia chini hadi juu ikiambatana na mazingira Bora kwa Mwalimu wa Shule ya Msingi, Kuleta vitabu vyenye tija, badala ya Hivi vya chenchi ya RADA ambavyo vina makosa MENGI MNO na haviendi na wakati.

Lakini pia hawashindwi kukurupuka na kuamua kuwasukuma Sekondari bila kurekebisha Ikama na kuongeza vifaa, majengo na vitendea kazi vingine kwa shule za sekondari ili ziwe na uwezo wa kupokea kundi kubwa la wanafunzi kutoka shule za msingi.

Ushauri:

1. Serikali irudishe KKK kuanzia darasa la Awali hadi III kabla hawajaamua kufuata ushauri wa HRW.
2. Ili kuingia Kidato cha Kwanza, mwanafunzi atapaswa kuhudhuria kozi ya kiingereza kwa mwaka mzima (BRIDGE COURSE) tayari kwa maandalizi ya kupokea masomo kwa njia ya Kiingereza au; Kubadili lugha ya kufundishia kuwa Kiswahili kwa masomo yote ya sekondari. Nawasilisha
 
Mm huwaga inanishangaza sana hii seriklai na wizara ya elimu hasa huyu waziri wa elimu
anaposema kuwa mwanafunzi wa daraja la nne aende kusomea ualimu sasa hapo tutawapataje
walimu walio bora kuweza kuwafundisha watoto wetu si yatakuwa majanga kama hayo
watoto watatoka kama wao walimu katika madaraja yao

wewe unafikiri kuwa mtoto anaweza kushika nafasi ya kwanza akifundishwa na mwalimu aliyeduni
kielimu sijui tufanyeje ili elimu yetu iwe juu kaitika kiwango kinachotakiwa?
 
Hii itakuwa kitu kipya.

Kwa bajeti gani elimu ya sekondari iwe haki kwa wote? SHule za kata tu zilizopo bado hazijapatiza ufumbuzi wa changamoto zinazokumbana nazo, walimu, nyumba vya madarasa, vifaa vya kufundishia, maktaba, maabara na vitabu. Pamoja na haya baadhi ys shule hizi zinalazimika kuchukua watoto hata wasiojua kusoma na kuandika vizuri, huyu mtu ndio umfundishe kusoma na kaundika afu aje aelewe kemia na fizikia?

Labda serikali pia ingefikiria kufufua lile somo la Self Reliance, walau watoto wakajua kujitegemea. Somo hili pia wakali-update kulingana na mazingira ya sasa, ka elimu ka ujasiriamali kakaongezwa.

Lakini pia vyuo vya VETA, vinaweza vikaangaliwa upya ni jinsi gani vitabeba wale ambao hawakupata nafasi ya kuedelea na sekodari, nao pia kozi zikaongeza kulingana na mazingira ya sasa.
 

You must be a great thinker!
 
ndio maana kwenye marekebisho yangu ya rasimu ya pili ibara ya 12(1)(e) nimeandika na ninataka serikali isiridhie mikataba ya kimataifa inayoenda kinyume na katiba yetu, ama sera zetu ama dira zetu,pia nimependekeza kuongezwa kwa ibara ndogo ya (3) kwenye ibara ya 115 ambacho kitakuwa ni kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (2)(g) kitakachozuia bunge kuridhia mkataba wowote unaoenda kinyume na katiba yetu ama sera zetu.

huu ni ujinga tunaaletewa, utafikiri marekani wanasoma wote bila kujali uwezo wa kusoma. badala ya kuboresha elimu na mazingira tunaambiwa wote waende, yaleyale ya kikwete kushauri mtihani wa kidato cha pili na la nne kufutwa alafu baadae wakarejesha
 
whaaaaaaaaaaaaaaaat? hiyo nchi gani? sijawahi kusomaa katika pitapita yangu walaa kusikia hiki kitu pamoja na kuwa nimfatiliaji, hebu nitajie nchi moja tu
 
hata hiyo ujerumani hawaendi wote, na sisi tukisema bure kama zamani hawataenda wote, yaani hawa wanachezea akili za watu, wao wamekazana kufanya tafiti alafu wanatuletea haki huku.
 
whaaaaaaaaaaaaaaaat? hiyo nchi gani? sijawahi kusomaa katika pitapita yangu walaa kusikia hiki kitu pamoja na kuwa nimfatiliaji, hebu nitajie nchi moja tu

china elimu ya chuo ni vya lazima wanatungia sera nowdays
 
china elimu ya chuo ni vya lazima wanatungia sera nowdays
ndio maana nilishangaa, navyojua mimi hakuna nchi hata moja duniani ambayo elimu ya lazima ni chuo kikuu, hata sasa nimesoma universal education ya china ni ya miaka tisa ambayo ina stage mbili primary na middle school na mwanafunzi anamaliza universal education akiwa na miaka 14 ama 15
 
Mkuu EMT ninaunga mkono hoja kuwa serikali isomeshe bure watoto wetu hadi sekondari yaani O level kwa sasa kwa kuwa facility za kuwafikisha A level hazipo. Hii ni haki yao maana mtoto anamaliza at 12-15 halafu anaishia mtaani hata ujuzi hana. Je huyo ataacha kuwa kibaka kweli? Je ataacha kubeba mimba za utotoni? Kama hi hivyo ile life expectancy itakuwaje maana mahitaji ya kijamii nayo ni duni sana. Hata hivyo kuna changamoto nyingi sana Tanzania kwa kuangalia machache kama ifuatavyo:

1. Shule nyingi za msingi hasa zile za serikali baadhi ya wanafunzi hawajui kusoma na kuandika!! Je kiingereza cha sekondari ni vipi? Hapa labda waseme wasome tu na hakuna mtihani wa kidato cha pili!!!! Watarudia wengi!!! Je resources zipo?

2. Je majengo ya sekondari ya kutosha yapo? Mwaka 2013 kuna wengi walifaulu ila waliachwa kwa kuwa hakuna majengo ya kutosha!!!

3. Waalimu janga la kitaifa!!! Wanasema ni wachache na ratio ya teacher:to pupil/students ni kubwa sana!!!! Wataleta waalimu wapi?
4. Ukiachilia mbali waalimu, je huduma nyingine kwa wanafunzi itakuwaje? mathalan masomo ya science maabara ni janga lingine.

5. Ili kuweza kusomesha watoto wetu hadi sekondari kwa Tanzania itachukua muda mrefu sana kutimiza ndoto zake maana sekta ya elimu ina changamoto nyingi sana.
Hayo ni machache sana niliyoweza kuangalia kwa haraka haraka ila nashauri utafiti wa kina ufanyike tena kubaini changamoto za mfumo huo na zifanyiwe kazi. Vinginevyo haiwezekani!!!! Universal Primary Education bado haijafanikiwa kwa 100%!!!! Ile michango kwa wazazi ambayo ni mikubwa kuliko ile ada ya kipindi kile imefanya watoto wengine wasisome!! Kutokana na umaskini!!! Fikiria mlinzi kwa mwezi 500, uji kwa siku 300-400 sawa na 1,500-2,000 kwa wiki!!! Tuition kulazimisha watoto wabaki 200-300 kwa siku sawa na 1,000-1500 kwa wiki!! Jumamosi kuna mitihani 1,000-2,000. Kwa mwezi jumla kati ya 14,500-22,500. Hii ni mifano tu!!!! Hakuna elimu bure kwa shule za msingi Tanzania. Hapo sijaweka gharama nyingine kwa wanaotumia usafiri wa daladala, sare, vitabu na madaftari!!! Je sekondari itawezekana?? Uzoefu huu ni kwa shule za serikali tu , binafsi hazihusiki!! Kwa walio na uwezo kifedha!!!! Universal Secondary Education in Tanzania, a dream yet to come!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…