Mitihani ya Dini kizungumkuti NECTA

Mitihani ya Dini kizungumkuti NECTA

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Safari hii ni Bible Knowledge na Islamic Knowledge. Mitihani hii miwili imezua sintofahamu na kusababisha matokeo ya Kidato cha Nne kuchelewa kutoka. Yalipaswa kutangazwa Jumatatu ya tarehe 11/2/2013. Yakataka kutokea ya mwaka jana.Lakini,NECTA imebaki salama.

Sintofahamu hiyo imetokana na kutofautiana kwa 'Marking Schemes' za masomo hayo zilizowasilishwa. Hivyobasi,mitihani hiyo ilisahihishwa kwa Marking Scheme zilizotengenezwa papo hapo. Hatahivyo,wataalamu wa dini zote walishirikishwa katika kuunda Marking Scheme hizo.Kila kitu kilikwenda sawa.

Mitihani imeshasahihishwa.Matokeo yameshapangwa.Yapo tayari.Ingawa si mazuri kwa Shule zetu za Serikali na hasa za Kata,yako njiani.Wasichana wamewafunika wavulana.Tayari kuwapa raha au karaha watahiniwa. Watahiniwa kaeni chonjo
.
 
Mkuu,ulipondwa sana humu kwa uzi wako wa awali. Yanaweza kutangazwa lini Mkuu?
 
Back
Top Bottom