Mitihani ya Taifa isiwe kipimo na njia pekee ya kuelekea mafaniko

Mitihani ya Taifa isiwe kipimo na njia pekee ya kuelekea mafaniko

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2012
Posts
5,351
Reaction score
7,639
Huu ni mtazamo wangu...

Mimi nadhani kupima uwezo wa wanyama wote kwa kuwaambia wapande mti ni kuwaonea baadhi yao, kwani kuna wanyama kama mamba watajiona wajinga maisha yao yote kwasababu kwa asili yao tu, hawawezi kupanda mti, wao ni wajuzi kwenye kupiga mbizi, halikadhalika, nyani watajiona werevu kwasababu kupanda na kuishi mitini ni asili yao.

Wenzetu wazungu humchunguza mtoto tangu anapokua, waki-notice anapenda kucheza na toys za magari wanaanza ku-suspect kwamba anaweza kuwa injinia wa magari au la, kuwa dereva, basi akishamaliza ile elementary/basic level ambayo ni sawa na o'level huku kwetu, humuendeleza kwny fani hizo.

My take: Kupima uwezo wa wanafunzi wote kwa Mitihani ya Taifa ni kuwaonea, wapo ambao watafeli na kujiona wajinga milele (WASIO NA UWEZO WA DARASANI-HAWA NAWAFANANISHA NA MAMBA), kumbe wangemaliza form 4 na kuendelezwa kwenye fani wanazozipenda na kuzimudu (kama za VETA) wangeweza kufanikiwa sana, lakini wapo ambao wataendelea kufaulu Mitihani ya NECTA (HAWA NAWAFANANISHA NA NYANI). Tusiwazuie, tuwaache wajiendeleze mpaka Vyuo Vikuu.
 
Back
Top Bottom