SoC02 Mitihani ya Taifa ni kikwazo kikuu kwa elimu bora Tanzania. Ifutwe kabisa

SoC02 Mitihani ya Taifa ni kikwazo kikuu kwa elimu bora Tanzania. Ifutwe kabisa

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
Mfumo wa elimu ya Tanzania ni mfumo ambao tangu nikiwa mdogo nimeukuta na hata wazazi wangu nao wameukuta hivyo hivyo na huenda hata watoto wetu wakaja kuuacha hivyo hivyo. Huu ni mfumo wa kikoloni, mfumo ambao umejikita sana kuandaa watoto kufauu mitihani ya Taifa, ni mfumo wa kushindanisha point, ni mfumo wa kushindanisha mashule, ni mfumo wa kushindanisha wilaya au mikoa.

Shule zote kwa sasa zimefungwa, ila unakuta Darasa la nne, Darasa la saba, kidato cha pili na kidato cha nne hawajafunga shule, hawa wanaendelea kwenda shule na wanaendelea kwenda shule kwa nini? Wanaandaliwa kwa ajili ya mitihani ya Taifa, hawa kwa sasa wana solve past paper mbali mbali ili basi ziwasaidie kupata maswali kwa ajili ya kuja kujibu mitihani ya Taifa, hawa watoto tangu January hawajapumzika ni mwendo wa kuandaliwa na mitihani ya Taifa sio kuandaliwa kutatua changamoto za kidunia hapana mitihani ya Taifa.Sio kuandaliwa kwamba wanaweza endana vipi na techinolojia ya sasa hapana ni kwa ajili ya kuja kuipatia shule husika div 1 za kutosha.

Shule ziko kwenye mashindano makubwa sana na kila shule inajua kabisa ikifaulisha watoto mwakani inapata watoto wapya wengi na hii ni biashara inayo lipa sana, hakuna shule inafaulisha watoto kujifurahisha bali ni kutafuta kupata wanafunzi wapya ili walete mapato shuleni.

Kwa nini huu mfumo haufai kabisa kwa Dunia ya sasa na ndo chanzo cha vijana kujaa mitaani na wamemaliza hadi kiadato cha sita wengine?

Shule nyingi zimejikita ku solve mitihani ilio pita ili watoto wanadaliwe kuja kujibu mtihani wa taifa, hakuna shule inawaaandaa watoto kuja kuingia mtaani bali wanaandaliwa kujibu mitihani ya Taifa, hii ni hatari sana kwa sasa ambapo Dunia isha shift kutoka huko ambako sisi tuna ng, ang,ania, Nchi nyingi sana ikiwemo hata Kenya zisha futa mitihani ya Taifa kwa sababu waliona imepitwa na wakati, Tanzania bado wazazi wako motivated na mitihani ya Ttaifa.

Chukua mtoto wako au wa ndugu yako alie faulu kidato cha 4 na kupta div 1 ya point 7 mwambia sasa iingie mtaani na aitumie hio div one yake kutatua changamoto zake na kujiletea maendeleo, huyo mtoto hakuna atakacho weza, huyo mototo pamoja na kupata div one ya point 7 hawezi survive mtaani kamwe kwa sababu ameandaliwa kujibu mitihani ya taifa.

Chukua mtoto wa kidato cha sita alie pata One ya point tatu na yeye mwambie sasa unaishia hapa ingia mtaani na tumia hio One yako kutatua changamoto, huyo mtoto hakuna atakacho weza na ana Div One ya point 3, hii ni hatari sana na sijui kama wazazi tunaliona hili, sijui kama tunao hii hatari kubwa sana kuliko hatari zote.

Kuna shule zinaingia hadi kwenye kuiba mitihani ili tu watoto wafaulu, kuna shule zinataka kuwafurahisha wazazi, kuna shule zinataka kuwafurahisha viongoi wa siasa na si vinginevyo hakuna shule ina muda wa kuwandaa watoto kuingia mtaani, wako makini na kuhakikisha wanafaulu mitihani ya taifa.

Nini kinaweza fanyika, ili basi kuandoa mashindano ya kukaririsha watoto na pia kuacha kuchosha watoto na kusoma mwaka mzima kisa wafaulu mitihani;

Mitihani ya Taifa ifutwe kabisa, ibakie mitihani ya levo za shule, ambayo itakuwa inasimamiwa ubora wake na maofisa wa elimu, ni kama ilivyo vyuo vikuu kila kimoja kina mitihani yake lakini ikiwa na ubora, hii itaondoa mashindano ya Div 1 na shule zitajikita kufundisha watoto kuelewa masomo na pia jinsi ya kutatua changamoto za kidunia, mithani ya ngazi za shule itaondoa biashara za kutafuta Div 1 ili watoto wafaulu na itajikita kuangazia uwezo wa mtoto.


Mfumo wa Competitive based curriculum(CBC) huu ni mfumo ambao Serikali inapaswa kuutumia, huu mfumo utapima watoto kwa uwezo wao binafisi na sio kwa mitihani, huu mfumo kila mtoto atapimwa na kutahiniwa kwa uwezo alio nao na sio kwa uwezo wa kukariri kama ilivyo sasa. Huu mfumo ndio hata Kenya wanautumia sasa na ndio sabau ya wao kufuta mitihani ya Taifa, na hata shule za International zinatumia pia huu mfumo wa CBC,hii inaweza andaa vijana kukabiliana na Dunia ya sasa na tofauti na ilivyo sasa ambapo motto anamaliza kidato cha 6 na ana Div 1 na bado hakuna anacho jua.

Div 1 za point 7 na 3 zilikuwa na thamani zamani ila sio leo hii, sio sasa, hii mifumo isha pitwa na wakati kitambo sana na inasikitisha sana Serikali bado imekumbatioa hii mifumo ya mitihani ya Taifa, hii mifumo ndo inazaa tuition, ndo inazaa shule kukusanya pesa nyingi za fomu na za kujiunga na shule na mwisho wa siku inachukau watoto kiduchu, angalia zile Seminary huwa ni jam kupata nafasi na kisa tu watoto wana faulu.

Wenzetu wako kwenye levo mabazo mtoto hata akiishia elimu ya chini bado kuna vitu anaweza fanya, kuna vitu kafundishwa shuleni na vinaweza msaidia, sisi still hadi leo tuna karirisha watoto kuchora ramani na mambo ya kilimo cha Mahindi Marekani.

Dunia ya sasa kukarisha watoto kuchora ramani za Africa ni ujinga mkubwa sana, yaani watoto wana karirishwa kuchora ramani wakati wenzao huko Asia wanafundishwa kuunda betri za simu, na cha ajabu wazazi tunashangilia eti mtoto wangu anajua kuchora ramani ya Africa.

Mbaya zaidi siku hizi unakuta hadi watoto wa vidudu au baby class wana shindanishwa na mitihani na wana hadi masomo ya ziada yaani tuition, na mazazi anapaswa kulipa pesa mtoto wake wa vidudu asome tuition na kweli mzazi analipa pesa, hii ni zaidi ya sijui ni seme nini.Mtoto anakuwa anacho jua ni mitihani basi.

Tunapaswa kuishinikiza Serikali iachane na huu mfumo wa kikoloni wa mitihani ya Taifa, mfumo ambao unawachimbia watoto kabuli, unaandaa watoto kuja kusajiri laini za simu mtaani, hio ndo vitu wanavyo toka navyo shuleni.

Competitive Based Curriculum ni mfumo ambao unaweza oko kizazi kabla ya kuwa too late ingawa poa tuko nyuma ya muda.

Karibuni
 
Upvote 5
Umeongea jambo la maana sana, mifumo ya mitihani ya Taifa isha pitwa na wakati tuko nyuma sana na ni kweli Wakenya wamefuta mitihani ya taifa na wamebakiza ya ngazi ya shule huko ndiko mtoto atapimwa uwezo wake na walimu wake. Tanzania bado raia wanaabudu sana matokeo hawajua madhara yake.
 
Aisee mimi naona ni vyema ungeitazama kwanza elimu ya kikoloni ilivyokuwa kiukwel huwezi kuilinganisha na ya sas maana elimu iliyotolewa wakati wa ukoloni ilijikita zaidi kufundisha stadi za maisha na ufundi mbalimbali hivyo basi, elimu ya sasa ni tofauti sana na ya kikoloni maana elimu ya sasa inamfanya mtoto afaulu mtihani na sii kufaulu maisha.
Ukipata nafasi pitia Makala yangu inayokwenda kwa jina la Elimu ya sasa haimkomboi kijana wa kitanzania, nadhani ukipitia vizuri utaweza kuona mambo mengi.
Ila kazi yako ni nzuri sema ulijichanganya tu kidogo pale kuhusu elimu wakati wa ukoloni
 
Aisee mimi naona ni vyema ungeitazama kwanza elimu ya kikoloni ilivyokuwa kiukwel huwezi kuilinganisha na ya sas maana elimu iliyotolewa wakati wa ukoloni ilijikita zaidi kufundisha stadi za maisha na ufundi mbalimbali hivyo basi, elimu ya sasa ni tofauti sana na ya kikoloni maana elimu ya sasa inamfanya mtoto afaulu mtihani na sii kufaulu maisha.
Ukipata nafasi pitia Makala yangu inayokwenda kwa jina la Elimu ya sasa haimkomboi kijana wa kitanzania, nadhani ukipitia vizuri utaweza kuona mambo mengi.
Ila kazi yako ni nzuri sema ulijichanganya tu kidogo pale kuhusu elimu wakati wa ukoloni
Mkuu nazungumzia mitihani ya Taifa, mataifa mengi sana hawana huo utaratibu, Unapo kuwa na mitihani ya Taifa una force au unakaribisha mashindano na dio kinacho fanyika, kuna raia wanazani kuplekea watoto Englisha medium ndo suluhisho sio kabisa kwa sababu tena huko ndio kuna pure competition. Wakenya kwa sasa hutasikia Tuition wala Top 10 students
 
O
Mkuu nazungumzia mitihani ya Taifa, mataifa mengi sana hawana huo utaratibu, Unapo kuwa na mitihani ya Taifa una force au unakaribisha mashindano na dio kinacho fanyika, kuna raia wanazani kuplekea watoto Englisha medium ndo suluhisho sio kabisa kwa sababu tena huko ndio kuna pure competition. Wakenya kwa sasa hutasikia Tuition wala Top 10
Sawa nmekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom