Mitindo ya nguo, nywele na viatu iliyovuma enzi zako

Mitindo ya nguo, nywele na viatu iliyovuma enzi zako

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Ukiacha raizon viatu, pekosi au bugaluu suruali, klimplin mashati na afro nywele miaka ile ya sabini, miaka ya tisini kuna mitindo ilivuma nikikumbuka huwa nacheka sana!

Unakumbuka :

Lakupanda-raba halafu gidamu zake ni rangi mbili tofauti chirimeni-magauni ready made yenye rangi kali sana.

Bio Act-suruali
 
dah!nimecheka mpaka bas,rangi kali ckuhz tunaita crazy colour!.....
 
mmesahau chupi ya VIP
ilikuwa ikikatika kule chini hii noma sana, sijui ziliishia wapi zile chupi ni nzuri sana bana
unatupia na raba mtoni
shati la kitenge
chupi ya jinja
 
Kuna mashati ya wanaume yalikuwa yanaitwa julianna. Kitambaa chepesi sana, see through. Kumbe jina lilianzia uganda, ukimwi uliitwa slim ama julianna. So mtu anaevaa nguo hizo see through alikuwa anaonekana kama carrier.

Ndaba, la kuchumpa.
Kuna jeans zilikuwa za bakabaka flani zinaitwa big sam.
 
Shuleni mlifundishwa kushona chupi ya jinja? Na kuweka kamba kiunoni ili iwe free size?
mmesahau chupi ya VIP
ilikuwa ikikatika kule chini hii noma sana, sijui ziliishia wapi zile chupi ni nzuri sana bana
unatupia na raba mtoni
shati la kitenge
chupi ya jinja
 
shati la juliana na mtindo wa kukata nywele push back. Pia carwash.
 
Aah,suruali za bioct,tokyo,savco,big sum,viatu vya mokasi,njumu za maradona(zilikuwa za vitambaa kigumu cheusi chini soli kama kiatu cha kusakata kabumbu na zilikuwa na majina ya wwahezaji tofauti.) kofia za Luck zilikuwa na bati juu na kwenye kenop ya mbele kuubwaa, redio ya mkulima band nne,betri unafunga kwenye box na mpira wa manati, redio ya casseti ya panasoni almaarufu redio ya memory ilikuwa na kitufe cha njano cha kurekodia, mashati ya juliana,bahama mama a.k.a ujiuji, mikanda ya suruali ya crocodile,kama hujatinga hui skull shauri yakooo! Mifuko ya kuwekea daftari ya sport,ilikuwa na kamba unabeba mgongoni kama kifurushi maana ilikuwa ni ya kunyonga, aaaaaaah long time agoo men! Wazee wa sukus star, sakayonsa,pomoni paka bushee,kwasakwasa,, ,
 
Enzi za Sansui disko Sea View, Go-Go disko Afrikana na The Sunburst bahari beach hotel (sunday school):

591565967_94a5364320.jpg

 
Shuleni mlifundishwa kushona chupi ya jinja? Na kuweka kamba kiunoni ili iwe free size?

hizi chupi sio zile zinawekwa lastic inaingizwa kwa kijiti mkwenye mzunguko wa kiuno halafu hiyo lasti inafungwa fundo saizi ya kiuno chako ukiona mpira unakubana unaongeza saizi? Maana hizi walikuwa wanatumia mpaka mpira wa manati.
 
Kichwani unakwenda kwa Afro!
Shati slim (lililobana) lawezakua la ndege au lisilo la ndege .
Usoni umepiga glass kama si gogoz basi Tv.
Mkononi saa Mortima .
Trouser bugaluu as known as pecoz ya kitambaa cha kabardin .
Down unakwenda kwa raizon ngazi mbili au 3 sana zikiuzwa Bora shoes sh 300 kwa 350 .
 
Back
Top Bottom