Pole sana kwa kuteswa na Pajero io, ambazo waswahili wanaziita GDI. Hizi ni gari nzuri sana na za kisasa, mafundi wengi wamezoea kubabaisha ndiyo maana watu wanadhani zina matatizo. Ningekushauri uipeleke Pugu Rd kwa mafundi wa Mitsubishi (Diamond Motors) au mafundi wa Bosch, wataangalia tatizo ni nini halafu watalitatua. Gari nyingi za kisasa (ikiwemo Pajero io) ziko sensitive sana kwa spark plugs na aina ya petrol, kwahiyo unapokuwa na gari hii uwe makini sana ili upate plug zinazofaa, kwasababu tatizo huanza baada ya kuweka plug zisizofaa, hata manufacturer wenyewe wa Mitsubishi wamekuwekea CAUTION kuhusu genuine plug katika cover ya engine.
Mimi ninayo pajero io, ilinisumbua kidogo nilipobadilisha plugs kwa mara ya kwanza, niliweka plug za kawaida ambazo zilikuwa hazichomi vizuri matokeo yake uchafu ukawa unajazana katika system ya air na vacuum sensor, baada ya kubadili plug na kusafisha system gari limerudi kuwa bomba kama mwanzo. Hata bei ya genuine plugs siyo mbaya, zipo NGK, BOSCH, nk.