Mitsubishi yakiri makosa kwa magari yake

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411


Mitsubishi imesema kuwa majaribio ya matumizi ya mafuta yalifanywa kwa njia isiyo sahihi.
Kampuni ya kuunda magari ya Japan ya Mitsubishi, imekiri kufanya makosa kwa tamwimu za matumizi ya mafuta kwa zaidi ya magari 600,000.

Mauzo ya hisa za kampuni hiyo yalifunga yakiwa yameshuka kwa asilimia 15 kutokana na ripoti kuwa ilikuwa imedanganya.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Mitsubishi ilisema kuwa majaribio ya matumizi ya mafuta kwa magari hayo yalikuwa yamefanywa kwa njia ambayo haikuwa sahihi.

Ilisema kuwa magari yaliyopatwa na kosoro hiyo yalikuwa yametengenezwa kwa kampuni ya Nissan.

Hayo yanajiri wiki sita baada ya kampuni ya magari ya Ujerumani ya Volkswagen, kukiri kudangaya katika mitambo ya gesi chafu ya magari yanayotumia mafuta ya diesel.

Chanzo: BBC Swahili
 
Kwa nchi zetu tunasubiri wenye nayo wakiri...maana tech ya kugundua hayo mambo sisi hatuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…