19 Oktoba 2020
Mkuranga, Pwani
Tanzania
Wakazi wa kata ya Tambani wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani, Tanzania wanalazimika kutumia mitumbwi kutoka eneo moja kwenda jingine baada ya daraja la Kifolongo kukatika.
Daraja hilo lilikatika Aprili, 2020 lakini mvua zilizonyesha kati ya Oktoba 13 hadi 18, 2020 zimesababisha maji kujaa eneo hilo na wananchi kulazimika kutumia mitumbwi kuvuka.
Katika mitumbwi hiyo wanafunzi wanatozwa Sh200 na watu wazima Sh300. Watu hulazimika kupanga foleni kusubiri mtumbwi mmoja ambao unatajwa kuwa salama zaidi kuliko mingine ambayo mara kadhaa ubinuka na kusababisha watu kutumbukia kwenye maji.
Source : Mwananchi Digital
Mkuranga, Pwani
Tanzania
MITUMBWI YATUMIKA KUVUSHA WANACHI MKURANGA