matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Wasalaam.
Mahubiri mengi kwa hawa mitume na manabii wa kisasa yamejaa uchonganishi, manipulation, saikolojia na neno kidogo. Mengine yote sinashida nayo shida ni hii ambayo pia hata waganga huwa wanafanya. Uchonganishi.
Yaani mtu anaenda kuombewa, muombewaji anaaminishwa kalogwa, mlogwaji anatajishwa aliyemloga wenda ni mjomba, boss, dada, kaka, mama au jirani.
Sasa huyu jirani sio muumini. Hii inaleta chuki, ugomvi, kuviziana na visasi baina ya ndugu na ndugu, ofisini, familia.
Jana nilikuwa napiga story na dreva mmoja anasema yeye alitajwa kuwa anamloga shemeji yake. Akafunga safari kwenda hapo kwa mtume karibu na mbezi ili kama kweli ni muhusika wamtoe huo uchawi. Cha ajabu alipowaeleza wapambe wakamwambia yeye hayamuhusu apotezee. Akasema jambo hilo limeleta mpasuko mkubwa kwenye familia anaonekana no freemason, mchawi na hafai hata simu haipokelewi. Wale machawa walipoona jamaa haelewi, walimuitia mabaunsa wakambeba na kumfukuza kabisa hilo eneo.
Inavyoonekana yule mtoto aliyemtaja no kama alipangwa ili kuvuta wakereketwa kupitia media. Muhusika kufirisika alifirisika kwa kujitakia na anasa, na kanisani haaminiwi anapunwa sadaka tu.
Haya makanisa kwa sababu yanakua kila kona, wote wanatumia tekniki za kùfanana wanaweza kusababisha uchonganishi wa kitaifa na hali ya kuchukiana na kuviziana ikarudisha nyuma kasi ya maendeleo.
Ni hayo tu.