John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Mitume wa Mwanzo Walivyoteswa na Kuuawa
Petro
Mtume Petro alikuwa kiongozi wa kanisa la kikristo. Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake.
Aliuawa huko ROMA, ITALIA.
Alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila, yeye alisulubiwa tofauti na Yesu Kkristo.
Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa ni kwa kichwa chini miguu juu katika msalaba. Hii ni kwa ombi lake yeye mwenyewe; hakutaka kusulubiwa kama Yesu.
Alisulubiwa kichwa chake kikiangalia chini kwa msalaba wa umbo la X kwa kutimiza unabii wa Yesu (Yohana 21:17-18).
Andrea
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Mtume huyu alihubiri injili katika inchi ya UGIRIKI. Alikufa kwa kusulubiwa kwa msalaba wa X, yaani mbao mbili zilisimikwa chini yake, akaangikwa ili afe polepole.
Walimfunga kwa kamba ili kumuongezea muda wa kuteseka. Ilichukua siku tatu akafa. Ila maajabu ni kuwa baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu kwa siku mbili hadi mauti ilipomchukua.
Yakobo Zebedayo
Alijulikana pia kama James. Mtume Yakobo alikuwa ni ndugu wa kunyonya wa Bwana Yesu (Mathayo 13:55). Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Alikuwa kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu nchini Israel ya sasa.
Alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo.
Mnara huo ni ule ambao shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe chini na Malaika wa Mungu watampokea, hivyo hataumia po pote.
Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha kutokea juu ya mnara, walimpiga na rungu lenye misumari, kumkatakata sehemu 28 tofauti mwilini na kisha kumkatwa kichwa huko JERUSALEMU. Alikuwa mtume wa kwanza kuuawa.
Yohana
Mtume huyu alikuwa mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Wakati wimbi kubwa la dhiki za wakristo likishamiri huko Roma, walimkamata Mtume Yohana na kumzamisha katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, Italia ya sasa. Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa. Mtume huyu alikatwa kichwa bila mafanikio ya watesaji, bila shingo lake kukatika. Alifungwa nyasi mwili mzima na kuchomwa moto, nyasi ziliungua lakini yeye na nguo zake hakuungua. Alipigwa mawe mpaka waliporidhika na kudhani kuwa amekufa, lakini aliinuka na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko katika kisiwa cha Patmos, Ugiriki, ili afie huko, kwani kisiwa kilikuwa kimejaa barafu na baridi, lakini hata hivyo mtume Yohana hakufa. Badala yake huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha Ufunuo wa Yohana.
Baadaye aliachiwa huru na kwenda kutumika kama askofu huko Uturuki ya sasa. Mtume Yohana baada ya kuhubiri injili, alikufa kifo cha kawaida huko EFESO, UTURUKI. Alifariki akiwa mzee sana. Ni mtume pekee aliyefariki bila mateso. Biblia inasema katika Matendo 12:1-2, kuwa mfalme Herode alimuua kwa upanga, alikatwa kichwa.
Filipo
Aliuawa kwa kusulibiwa alipokuwa akiitaabikia injili huko kaskazini mwa Uturuki. Alikamatwa kwanza na kutupwa gerezani, kisha baadaye wakamsulubisha na kutungika kwenye msalaba nchini MISRI.
Bartholomeo
Alijulikana pia kama Nathanieli. Alikuwa ni mumishenari huko Asia ya sasa. Alihubiri injili huko India, Pathia, Arabia na Armenia.
Alipokuwa huko Armenia ndipo alipopata mateso mengi sana kwa ajili ya imani ya kiristo na jina la Yesu. Mtume huyu alikuwa na mke mmoja na watoto wawili wa kike. Mmoja alikuwa ni muombaji na mwingine alikuwa mwimbaji. Bartholomeo alivuliwa nguo zote huko Armania na kukatwa mshipa wa damu kwenye mkono wake. Kisha damu yake ilikingwa kwenye glasi mbili na kupewa mkewe anywe. Baada ya kumaliza kunywa damu ya mume wake, akasema maneno haya “mume wangu jipe moyo, mimi natangulia kwa baba”, kisha akaanguka chini, akafa.
Bartholomeo aliuawa baada ya kugoma kuacha mafundisho yake ya kanisa. Alichapwa kwa mijeledi mikali, akachunwa ngozi akiwa hai, akakatwa kichwa, kisha kutundikwa msalabani kichwa chini mguu juu, huko ARMENIA.
Thomas
Aliuawa kwa kuchomwa mikuki na maaskari wanne mgongoni na kutokezea tumboni huko INDIA, katika safari zake kama mumisionari wa makanisa ya huko India.
Mathayo
Alijulikana pia kama Lawi. Mtume huyu ni yule ambaye alikuwa mtoza ushuru (Mathayo 9:9-11). Alihubiri maeneo mbalimbali huko Jerusalem, Italia, Ethiopia na Iran.
Aliuawa kwa upanga kwenye madhabahu kanisani, baada ya kuonesha imani kali kwa kanisa la Kristo. Alikufa kwa kuuawa kwa upanga mbali kidogo na mji mmoja nchini ETHIOPIA, akiwa kanisani. Mfalme huko Ethiopia alimtamani mpwa wake mwenyewe ambaye tayari alikuwa mtawa, lakini Mathayo alimkemea vikali. Ndipo mfalme alitoa amri ya kuuawa kwake. Kwanza alipigwa kwa muda mrefu, na baadaye akakatwa kichwa.
Yakobo wa Alfayo
Alitupwa kutoka kwenye kinara na kisha kupigwa na rungu lenye misumari hadi kufa huko JERUSALEMU.
Simoni Zelote
Alihubiri injili Mauritania na baadaye Uingereza, kisha akaenda IRAN ya leo, ambako alikatwa katika vipande viwili kwa kutumia msumeno.
Yuda Thadayo
Alipigwa kwa rungu hadi kufa, kisha akakatwa kichwa kwa kutumia shoka, huko nchini ARMENIA ya leo.
Yuda Iskarioti
Mtume huyu alijinyonga huko JERUSALEMU baada ya kupata maumivu makali ya kumsaliti Yesu kwa vipande 30 vya fedha.
Alikwenda bondeni, kisha akapanda juu sana, na kujinyonga huko. Baadaye, kamba ilipokosa nguvu, mwili wake ukadondoka chini bondeni kwa kasi sana, ukitanguliza kichwa. Tumbo lake lilipopiga chini, matumbo yake yote yalitoka nje, akafa.
Mathiya
Huyu ndiye mtume aliyechukua nafasi ya Yuda Iskarioti aliyemsaliti Yesu. Yeye alipigwa kwa mawe na mwishowe kukatwa kichwa huko JERUSALEMU.
Paulo
Huyu hakuwa miongoni mwa mitume kumi na wawili wa mwanzo kabisa. Alipata upofu wa ghafla kutokana na kupigwa na mwanga mkali, akiwa njiani kwenda Misri ya leo, kufuata waumini ili kuwapeleka Jerusalem kwa ajili ya kuwatesa na kuwasulubisha. Yaani, alikuwa adui wa ukristo. Wakati mwanga huo ukimtokea, alisikia sauti ya Yesu ikimwambia “kwa nini unanitesa?”. Kuanzia hapo aliongoka, na kwa jinsi hiyo akawa mtume mteuliwa, na kuanza kuhubiri neno la Kristo kwa nguvu zake zote. Mtume Paulo ni mtume pekee ambaye alifanya kazi kuliko wote waliomtangulia. Alikaa gerezani mara nyingi zaidi. Kwa Wayahudi, mara tano alipata mapigo 39. Mara tatu alipigwa kwa bakora, mara moja alipigwa kwa mawe, mara tatu alivunjikiwa jahazi, kuchwa kucha alipata kukaa baharini. Aliuawa nje ya kuta za ROMA kwa kukatwa kichwa.
Hivyo ndivyo mitume wa mwanzo wa Yesu Kristo walivyoteswa na kuuawa, mashujaa wa imani ya Kristo.
Ilikuwa ni mateso makali kupita kawaida. Lakini, kwa imani na Kristo, walivumilia yote na kufa kishujaa. Hakuna kinachoshindikana, ni bidii yako na imani yako tu kwa Mungu wa kweli.