Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Hapo ni Bugando hospital,imeonekana mitungi inayosemekana ni ya Oksijen ikishushwa.
Ikumbukwe wiki hii nzima kumekuwa na kelele nyingi mitandaoni kuhusiana na ukosefu wa au upungufu wa mitungi hiyo katika hospitali hii na nyinginezo. Ni imani yetu Serikali imelisikia hilo na kulitatua haraka sana.
Kama mwanabodi naipongeza Serikali ya mama Samia kwa kulitatua hili kwa haraka sana, lakini tuendelee kumkumbusha pia aendelee kukubali kukosolewa na watu kuwa huru kutoa taarifa/maoni mbalimbali za msingi na maslahi mapana kwa jamii.
Yasiwe kama ya yule aliyetaka kumpa shuruba raia aliyetoa taarifa ya "ufa wa majengo ya udom" au "ubovu wa barabara kule mbugani"
Kutoka Sabasaba live kwenye uzinduzi wa Tela za Punda ni mimi Shujaa.
=====
Bugando yapokea mitungi 300 ya Gesi, kukabili corona
Hatimaye hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando ya jijini Mwanza imepata msaada wa mitungi 300 ya gesi kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya upumuaji wakiwemo wa corona
Akizungumza na Nipashe ofisini kwake, Kaimu Mkurugenzi wa Bugando, Dk Fabian Massaga amesema mitungi hiyo imetolewa na Bohari Kuu ya Madawa (MSD).
Zaidi, soma: Hospitali ya Bugando yakumbwa na upungufu wa mitungi ya Oksijeni kwa Wagonjwa wa Kupumua