KERO Miundombinu mibaya ya choo Stendi ya Bweri (Musoma)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Natoa rai kwa mamlaka husika kufuatilia hali mbaya ya miundombinu ya choo katika stand ya Bweri Musoma. Vyoo hivyo vimekuwa kitishio kwa afya na usalama wa watumiaji kutokana na uchafu na ukosefu mkubwa wa maji ndani ya vyoo.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba maji huwekwa kwenye vyombo maalum, na yakisha hakuna huduma nyingine ya maji inayopatikana hali inayowalazimu wananchi kutumia vyoo katika mazingira magumu sana.

Stand ni eneo linalotumiwa na watu wengi kila siku, hivyo ni muhimu kuboresha huduma hii haraka ili kuepusha madhara ya kiafya na kulinda hadhi ya abiria pamoja na wananchi wanaotumia stand hiyo. Tunaomba hatua zichukuliwe mapema.

 
Dah nilikutumia wakati natoka musoma to Dar hali ya hivyo vyoo ni mbaya sana sijui pesa wanaochaji inaenda wapi isifanye ukarabati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…