SoC04 Miundombinu wezeshi ni chanzo halisi cha ukusanyaji na upatikanaji wa kodi hifadhi ya mlima Kilimanjaro (kwa serikali)

SoC04 Miundombinu wezeshi ni chanzo halisi cha ukusanyaji na upatikanaji wa kodi hifadhi ya mlima Kilimanjaro (kwa serikali)

Tanzania Tuitakayo competition threads

Nelly shayo

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
5
Reaction score
1
Hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Tanzania ni moja ya hifadhi kubwa na ya umuhimu zaidi katika nchi ya Tanzania na Afrika kwa ujumla. Hifadhi hii ipo mkoani Kilimanjaro ikizungukwa na wilaya zake zaidi ya tano ambazo ndio inakopita hifadhi hiyo ikiwa na njia zake za kupandia. Wilaya hizo ni siha(lemosho gate) Hai(Machame gate) moshi mjini (mweka gate) Rombo (Rongai gate) na Moshi vijijini (marangu gate).

Hifadhi hii ya mlima Kilimanjaro Tanzania inaiingizia serikali pato la nchi kutokana na watalii kuja kuupanda na kuutazama mlima Kilimanjaro pamoja na mimea inayopatikana katika mlima huo. Kutokana na faida hizo lukuki haswa kwenye pato la serikali ni wakati sasa wa serikali kuangalia namna za kuboresha miundombinu inayosaidia zoezi la utalii katika mlima huo ili kuwavutia wageni wengi zaidi kuja kutalii na kutengeneza fedha zaidi kwa nchi. Hivyo nashauri yafuatayo;

1. Kutengeneza barabara za kisasa haswa zinazoelekea kwenye malango (gates) ya kupandia mlima huo. Mfano njia ya kupandia ya lemosho iliyopo wilayani siha ni mbaya kiasi kwamba wageni hulazimika kuanza safari kwa miguu nje ya eneo rasmi linalotakiwa kuanzia safari. Hivyo wageni hutafsiri kama ni ukarimu(hospitality) mdogo pamoja na huduma mbaya. Wageni hupungua kwa adha hii na mapato hupungua pia kwa serikali.

2.Kujenga hoteli za kisasa zenye hadhi ya nyota tano zinazoweza kulaza wageni wengi. Hii tumeshuhudia kwa miaka mingi wageni wengi huja kutalii na kushukia nchi jirani ya kenya kwani hukosa hoteli za kisasa za kulala. Hivyo sisi Taifa kuingia hasara ya kupoteza pato ambalo lingetokana na wageni kulala kwenye hoteli za ndani.

3.Kampeni wezeshi ni chanzo cha ongezeko la wageni wengi zaidi. Ni kweli kuwa kampeni nyingi za kuutangaza mlima Kilimanjaro kwingineko kunasaidia ongezeko la wageni wengi zaidi kuja kutalii, hivyo serikali pamoja na makundi binafsi yanatakiwa kupromote mlima Kilimanjaro kama kitovu cha utalii ili wageni waje wengi zaidi. Mfano Tanzania Royal Tour Hiyo itasaidia wageni wengi kuja kutalii na kukusanya mapato zaidi kwa nchi.

4.Kusimamia upatikanaji wa waongoza utalii wenye hadhi sawa na kazi husika(tour guide and operater) pia serikali inatakiwa kuhakikisha waongoza utalii katika hifadhi wanakidhi sifa zote kusudi kufanya wageni wanayafurahia mazingira yote ya safari kwani waongoza watalii wengine hushindwa hata kujieleza vizuri katika lugha ya wageni husika. Pia wapishi hushindwa kuwapikia wageni chakula wanachokihitaji husababisha wengine kurudi nusu ya safari. Hii hodhorotesha namba ya wageni ambao wangetamani kuja kutalii kwani hushindwa kuyafurahia mazingira kulingana na wanayoyasikia kutoka kwa wenzao

5.Kuhakikisha unadhifu, ulinzi wa wageni. Jukumu hili ni muhimu zaidi kwani wageni huja na fedha nyingi za kusafiria, kulipia mishahara,kodi na kula. Hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha wageni wanaokuja wanalindwa wao kama wao na vitu vyote walivyonavyo. Hii itawapa sura nzuri katika kuiongelea hifadhi hii na kuongeza wageni zaidi.

#Mwisho. Serikali kama mmiliki wa hifadhi ndio mwenye jukumu kuu zaidi la kusimamia, kuongoza na kuboresha zaidi mazingira katika hifadhi hii kusudi kujikusanyia pato zaidi, japokuwa mashirika binafsi wanaweza kusaidia katika upatikanaji wa tour guides wenye viwango, ujenzi wa hoteli za kisasa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom