SoC04 Miundombinu yetu na ajali za uso kwa uso

SoC04 Miundombinu yetu na ajali za uso kwa uso

Tanzania Tuitakayo competition threads

Omolo

New Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
3
Reaction score
3
Nchi yoyote ile ili iwe na uchumi imara inatakiwa kuwa na miundombinu ya uhakika kwa ajili ya usafirishaji, usambazaji wa bidhaa kutoka eneo moja kwenda jingine.

1: Katika Tanzania tuitakayo tunataka kuona kwamba kuna miundombinu imara hususan barabara, Leo nataka kuongelea miundombinu ya barabara ambayo Mara nyingi imekuwa ikisababisha ajali za mara kwa mara hasa barabara zetu, mifano ya barabara ambazo zimekuwa na ajali za uso kwa uso kutokana na njia moja, barabara hizo ni kama za kutoka Dar kupitia Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Tinde, Kahama, Nyakanazi, Rusumo hadi nchi jirani za jumuiya ya Afrika mashariki, pia kuna barabara ya Kutoka Arusha, Babati, Singida Kupitia Sekenke hadi Tabora. Bila kusahau barabara ya Dar Mbeya au Mwanza mpaka Mbeya. Mara nyingi hizi barabara zimekuwa zikitumiwa na Magari ya abiria (Mabasi, Coaster, haice n.k) na Magari ya mizigo (Mafuso , Semi trailer, Magari yale ya kusafirisha mafuta n.k).

Napendekeza Tanzania tuitakayo kufikia 2050 tuwe na njia nne kwenye hizo barabara zetu kuu za Afrika mashariki, njia mbili za kwenda yaani (two ways⬆️⬆️) na njia mbili za kurudi (two ways ⬇️⬇️) hii itapunguza ajali za uso kwa uso ambazo zimekuwa zikisababisha na baadhi ya Malori ya mizigo, pamoja na kupungua foleni na msongamano wa magari sehemu ambazo ni korofi, kupitia andiko hili nashauri serikali ya Tanzania kushirikiana na serikali zote za jumuiya ya Afrika mashariki waje na mkakati wa pamoja wa kujenga barabara za njia nne ili kupunguza vifo, nguvu kazi za taifa kupotea, na ulemavu unaosababishwa na ajali za mara kwa Mara.

2: Pia napendekeza Tanzania tuitakayo baada ya miaka 15 ijayo kuwepo kwa Kamera za CCTV kufungwa kwenye hizi barabara ili kubaini madereva wazembe na kuchukuliwa hatua za kisheria pindi wanapokiuka sheria za usalama barabarani.

3: Kupitia ajali za mara kwa mara kupitia hizo barabara, napendekeza Tanzania tuitakayo kufikia mwaka 2045 tuwe na magari mengi ya zimamoto na uokoaji kwa kila kata, kwani mara nyingi inapotea majanga kama ya moto au yale yanayohitaji uokoaji unakuta kuna umbali mrefu kutoka eneo la tukio hadi sehemu ambapo kuna hizo vyombo vya zimamoto na uokoaji, hivyo ni jukumu la serikali sasa kusomesha wataalamu wa kutosha na kununua vifaa vya kutosha kwa ajili ya jeshi la zimamoto na uokoaji, kwa kufanya hivyo tutapunguza na kuokoa sehemu za mali, vitu na maisha ya watu kwa kuwa jeshi letu litafika eneo la tukio kwa wakati.

4: Napendekeza Tanzania tuitakayo kufikia mwaka 2040 kununua magari ya kubeba wagonjwa maarufu kama ambulensi ili kuokoa maisha ya watu pale panapotokea ajali, Magari haya yakiwa mengi kiasi cha kila kata kuwa na magari zaidi ya mawili itasaidia inapotokea ajali watafika kwa wakati na kuchukua majeruhi na kukimbiza hospitali haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya watu.

5: Kuwepo kwa mfuko wa dharura ya ajili ya kukarabati miundombinu ya barabara hasa kipindi cha mvua, napendekeza Tanzania tuitakayo kufikia mwaka 2030 tuwe na mfuko rasmi kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu kama vile madaraja, makaravati na barabara zenyewe pale inapotokea mawasiliano ya barabara kukatika, hii itapelekea miundombinu hiyo kurejeshwa kwa wakati pasipo kusubiri fedha kutoka kwenye fungu fulani, tunataka kuona Tanzania tuitakayo ikifa na mafanikio makubwa kwenye sekta ya miundombinu na kupunguza ajali za mara kwa mara hasa yale yanayohusisha ajali za uso kwa uso.

Asanteni naomba kuwasilisha.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom