Nyakarungu
JF-Expert Member
- May 1, 2011
- 472
- 377
[h=5]KUTOKA MOYONI MWANGU, KUHUSU MIVUTANO YA KATIBA MPYA!
Soma kwa makini sana UELEWE!
Serikali ya tanganyika ilikuwepo na ikamezwa na muungano, ili kuleta balance hakukuwa na namna zaidi ya kulifunika jina la Tanganyika.
Kwa sasa wapo watu wanaodai serikali ya tanganyika, ukiwauliza wamekosa nini kwa kutokuwepo jina la tanganyika, hakuna jibu zaidi ya kutaka kutajwa kwa jina hilo tu, ambalo kwa sasa halipo kiumbo lakini kiuhalisia Tanganyika ipo na ndio inayoendesha Tanzania.
Wapo Wanaodai serikali yenye dola kamili, yaani tafasiri halisi ni kuwa kusiwepo na muungano tena, mamlaka ya muungano iwe mtumwa wa serikali hizi mbili ndicho wakitakacho wazanzibar, wakidai kuwa tanganyika imewakandamiza na hata hivyo hawataki serikali tatu tu, bali wao shida yao ni dola kamili ya zenji.
WANASIASA
CUF, wanahitaji serikali tatu wakiamini watapata ushindi wa kuongoza serikali ya zanzibar, wakiamini kuwa ccm haitakuwa na nguvu ya ushawishi kwa zanzibar ikiwa katka hali ya serikali tatu (pengine ni kweli na wanaweza kufanikiwa kwa sababu hii)
CHADEMA, wanahitaji serikali tatu, miongoni mwao wapo wanaoidai tanganyika kwa maana ile niliyoitaja hapo juu kuwa wao furaha yao ni kuwepo kwa jina la tanganyika tu na sio kwamba wanajua kuwa tanganyika ndio hii inayoendelea sasa na wala hawana sababu za kuidai wala hawana hitaji la kuwa wanavitu wanavikosa kwa kukosa jina hilo.
Lakini wapo humohumo wanaopiga hesabu za kisiasa na kupata jibu kuwa ccm inafaidika sana na kura za wazanzibar na kwa kuwa chadema yenyewe haina ushawishi na imeshindwa kufanikisha hilo visiwani kwa hiyo ni bora ipatikane serikali tatu ili balance iwepo na ikiwezekana kura za zanzibar ccm zipungue, yamkini watafanikiwa kupata ushindi katika uchaguzi ( kwa hilo bado ni mtihani kwani mpaka sasa takwimu za ccm ni kubwa kulinganisha na chadema huku bara, labda ifikapo 2015 mambo yawe yamebadilika)
CCM , wao nao wamegawanyika makundi mawili, kwa kuwa wote wanapaza sauti za kuitaka katiba iweke muundo wa serikali mbili,
Lakini walioasisi mjadala na kuamua kupigia debe serikali mbili ni wenye ufahamu juu ya siri ya muungano, na wenye kuona ukweli kabisa na hatari ya kuvunjika kwake kama kukiwekwa serikali tatu ambazo zitarahisisha zanzibar itengeneze dola kamili kama inavyodai kwa sasa
kundi la pili ni wanachama na washabiki wanaounga mkono hoja za wakubwa wao, yaani hakuna mwanachama anaefurahi endapo hoja ya chama chake itashindwa na ya chama kingine.
Mwisho kabisa, naupongeza muungano wa vyama vya upinzani, lakini nikiwashauri kuelewa maana halisi ya demokrasia, kwani unapokubali kuingia kwenye uringo wa demokrasia ukubali kushinda au kushindwa.
Maana ya demokraisa sio kuwa mdogo tu ashinde, bali ni kuwa mmoja ashinde.
Hata kwa zengwe mradi ameshinda kwa kura, zengwe ni kiungo mojawapo cha demokraisa ya afrika na ndio sababu hata kwenye chaguzi za vyama vya tanzania kiungo hiki cha zengwe huchukua nafasi kubwa sana.
Na Grayson M. Nyakarungu
KITABU CHA PRACTICE WHAT YOU PREACH KIKO MADUKANI SASA[/h]