msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 842
- 1,197
Na Queen Lazaro
Ni wazi kwamba elimu ndio msingi wa nchi yoyote Duniani iliyoendelea, inayoendelea au inayotaka kuendelea hasa katika zama hizi za sasa ambapo Teknolojia imeshika kasi kwani kufanya maendeleo kwa watu wasioelimika ni sawa na kazi bure yaani kubeba maji kwenye gunia.
Nchini Tanzania Serikali ya awamu ya sita tangu iingie madarakani imeboresha kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu na kubwa zaidi ni elimu bure ili kutoa nafasi kwa kundi kubwa la watoto kupata elimu ambao ndio Taifa la kesho linalotarajiwa kuendeleza mazuri yanayofanywa sasa.
Mbali tu na kuwekeza kwenye elimu kuanzia ngazi ya awali, msingi, sekondari na elimu ya chuo kikuu bado ikaonekana haja ya kuongeza nguvu kwenye elimu ya ufundi Stadi yaani VETA ili kusaidia Taifa kufikia azma yake ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Hivi karibuni Serikali imetenga zaidi ya Bilioni 100 kwa ajili ya kuanza kujenga vyuo vya ufundi stadi katika Wilaya 63 ambazo hazina vyuo hivyo.
Serikali inatambua umuhimu wa kukamilisha Ujenzi huo ili itoe mafunzo yatakayowawezesha vijana kujiajiri na kuajiriwa. Kubwa kuliko hivi karibuni Rais Samia atakabidhiwa Rasimu ya mitaala mipya ambayo imekuwa ikiandaliwa na Taasisi ya elimu Tanzania TET.