Miyeyusho ya Wahubiri Injili wa kisasa inahitaji kukosa D mbili kuwaamini

Miyeyusho ya Wahubiri Injili wa kisasa inahitaji kukosa D mbili kuwaamini

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Mshirika akiwa na uhitaji wa pesa anaambiwa inabidi aombwe maombi apate pesa au mafanikio lakini wahubiri wenyewe wa kisasa wakitaka pesa wanasisitiza sana washirika wamtolee mungu matoleo ya sadaka, Sasa kwa nini na wao wenyewe wasiombe na kumsubiria mungu awape baraka.

Kuna wengine wanatembea na bodyguards mabaunsa huku wanasisitiza sana mungu ndiye mlinzi wa watu wake.

Wengi ni matajiri wanaishi maisha ya anasa huku wanahubiri injili ya mtu aliyekuwa masikini na wanaohubiriwa wenyewe ni mafukara malofa wa kutupwa.
 
Mtu mvivu wa kusoma Bible si mtaji wa matapeli wa kidini pekee hata waganga wa kienyeji,kifupi ukiitelekeza bible wewe ni punching bag,utapasuka sana.
 
Mshirika akiwa na uhitaji wa pesa anaambiwa inabidi aombwe maombi apate pesa au mafanikio lakini wahubiri wenyewe wa kisasa wakitaka pesa wanasisitiza sana washirika wamtolee mungu matoleo ya sadaka...
Maandiko Yako wazi, watu wangu waangamia kwa kukosa maarifa!Si wote waniutao Bwana Bwana wanafundisha yaliyo ya kweli. Hata shetani hujigeuza malaika wa Nuru.
 
Ni huzuni Kwa kweli,Watu wamegeuka misukule ya manabii hawasikii,hawaambiliki Imani Yao wameielekeza Kwa manabii!
 
Wanahubiri mafanikio ya kimwili na sio kiroho .

Then watu wavivu kusoma neno ndo hudanganywa kirahisi na manabii wa uongo.

Ukiachana na bible na quruan MTU Anabadi kujielimisha zaidi kuhusu how to get (Sipiritual power ).
 
Kapu La Mjinga Sasa Mwelevu Anatia Mkono Tu
 
esa au mafanikio lakini wahubiri wenyewe wa kisasa wakitaka pesa wanasisitiza sana washirika wamtolee mungu matoleo ya sadaka, Sasa kwa nini na wao wenyewe wasiombe na kumsubiria mungu awape baraka.
Wao walimuomba Mungu awape watu ili hao watu Wamsaidie kuipeleka Injili Mbele. ni kama Serikali inawataka Mulipe Kodi ili wawaletee maendeleo ila wao wanaishi kwa anasa sana na hizo kodi zenu.
Kuna wengine wanatembea na bodyguards mabaunsa huku wanasisitiza sana mungu ndiye mlinzi wa watu wake.
Mungu analinda Roho sio mwili. hata Yesu alikuwa na wanafunzi Kumi na wawili hao ndio walikuwa wanamlinda. Mlinzi mmoja alimkata sikio askari waliokuja Kumkata Yesu.
Wengi ni matajiri wanaishi maisha ya anasa huku wanahubiri injili ya mtu aliyekuwa masikini na wanaohubiriwa wenyewe ni mafukara malofa wa kutupwa
Wa madhabahuni wanakula madhabahuni. Usije kujidanganya kuna mtumishi eti anaishi kwa anasa. Maisha yao ni ya Kujinyima sana.

MWISHO UKIONA NI RAHISI KAFANYE NA WEWE
 
Back
Top Bottom