Ndugu wana JF.
Nimepokea bila mshituko wala msisimko wowote kuwa Mizengo Pinda ameteuliwa kuwa PM.
Kimsingi Pinda ni muadilifu na ana haiba ya 'mtu mwenye kutenda haki'. Tatizo la Pinda ni moja tu: Ni muoga. Chaguo sahihi la mafisadi. Wanataka mtu anayeweza kulia na kutoa machozi kama mtoto mdogo bungeni. PM ambaye mafisadi wakimuamuru 'sema meremeta ni ishu ya JWTZ' akubali na aseme. Au fisadi akimtuma 'muambie Zitto Kabwe hatorudi Bungeni 2010' anasema kweli. Aibu ya TZ.
Tangu ateuliwe 2008, amedhihirisha kuwa ni muoga na kwa hiyo amewafanya WaTZ wakichukie chama chake kwa sababu siyo jasiri. Hawezi kuthubutu. Nathubutu kusema bora Lowasa kuliko Pinda. Ubaya wa Lowasa ni tabia yake ya kufanya ubia na wahujumu uchumi....Wahindi.
Kwa kifupi kuteuliwa kwa Pinda ni muendelezo wa kiduku.
Makinda TV.
Hii ni runinga. Tena runinga ya mbao. Kazi ya huyu maza ni kutafuta vifungu vya kulisha 'ban' wabunge watakao chokonoa maslahi ya waliomuweka. Aibu yetu. Aibu ya Tz.
Skizia baraza la mawaziri. Usishangae kuyakuta majina yafuatayo:
- Makongolo Mahanga (PhD feki)
- Zakhia Meghji (WaTz wamesahau madudu yake akiwa hazina)
- Lawrence Masha (rafiki na kipenzi cha familia)
Kama kawaida. Mkwere anaendeleza harakati zake za usanii kwenye uongozi wa nchi. Katika Zama hizi ambapo Watanzania wanataka viongozi wanauthubutu.
Ndiyo maana mimi ni mfuasi wa Chadema kwa sababu viongozi wake wanathubutu.
Sasa tunaletewa mtu anayetumwa, tena na mafisadi, "kaseme hivi...". Kazi ipo.
Ndiyo maana nathubutu kuuliza,
Pinda ni bora kuliko Dr. John Pombe Magufuli?
Nisaidieni.