Ambiele Kiviele
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 15,267
- 29,917
[emoji95]MIZIGO TULIYOIBEBA AMBAYO HAINA ULAZIMA WALA FAIDA[emoji95]:-
1.[emoji95]Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa
maisha ya wengine na umesahau maisha yako.
2.[emoji95]Umebeba vinyongo na visasi moyoni
vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi
kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.
3.[emoji95] Una marafiki wengi ambao ni kama kupe,
wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika
maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako
karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!
4.[emoji95]Umeweka mbele zaidi "watu watanichukuliaj
e" kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio
wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na
unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna
uwezo huo.
5.[emoji95]Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo
hakuna.Unatamani mafanikio tu moyoni lakini
huna mipango ya kuyafikia.
6.[emoji95]Maisha yako yote umeyaweka kwenye
mitandao ya kijamii.Huna siri hata moja!Hivyo
unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo
yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka
kwenye mitandao ya jamii kwa sababu
ukibadilika tu watasema "umefulia"
7.[emoji95]Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni
mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na
kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na
mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya
kujuana nao.
8.[emoji95]Upo sahihi kila siku(you are always right).
Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa
mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi
na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku
kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia
"hapa umekosea" kwa sababu ya ujuaji wako.
9.[emoji95]Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho
kusoma kitabu ilikuwa ni "Ngoswe, penzi kitovu
cha uzembe" Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa
ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi "life skills"
wala ujuzi mwingine.
10.[emoji95]Unazurura mno mitandaoni bila faida.
Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu
na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu
umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata
shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya
vocha.
ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli unahitaji
kusonga mbele!
Shtuka[emoji33]
Jamanikijani festival hiyooooo!!!!