wanandugu nimeamua kulima alizeti katika kiwango kidogo (ekari 5) kwa majaribio katika maeneo ya Fukayosi- Bagamoyo. sasa kwa sababu alizeti zina maua mengi naona ni vema niyatumie kwa ajili ya uzalishaji asali pia.
sasa ndugu zangu najua mizinga inapatikana SUA.lakini hapa kwa Dar es salaam unaweza kuipata wapi.. kuna mtu kaniambia SIDO ila sina contacts. naomba mwenye contacts za wapi naweza kupata mizinga ya nyuki pamoja na mtaalamu wa kunielekeza naomba anisaidie.
thanks
wizara ya maliasili pale kawawa road/pugu road.near bohari ya serikali wanatoa elimu ya nyuki plus mizinga.kuna thread ya nyuma kidogo,malila alizungumzia kuna sehemu wanauza mizinga bei poa sana.ipo iringa 🙂 all the best
hivi maua ya alizeti huwa yana contribute kwenye asali? nijuavyo mimi si maua yote. watch seasons pia maana si wakati wote nyuki wanatengeneza asali. inawezekana wakati wa maua ya alizeti nyuki wanakuwa likizo, na ikaishia kula kwako.