JonesLuba
Member
- Sep 26, 2021
- 5
- 3
Ni alasiri ya saa tisa mchana. “Hii nchi ilipofikia! Ila, ngoja tuvune tulichopanda”, maneno haya yanatoka kwa baba yangu, ambaye ameketi sebuleni akipata chakula cha mchana. Hii ni baada ya kupokea ripoti ya matumizi na mapato kutoka ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali.
Ripoti ambayo ndani yake imesheheni matumizi mabaya ya fedha za umma, ubadhilifu na wizi. Ninasimama kwa muda kidogo, kwa lengo la kusikia mwendelezo wa kulalamika kwake. Baada ya kujibiwa kwa ukimya, naelekea chumbani na kujitupa kitandani. Akilini mwangu, maswali yanaanza kujengeka. Ni nini tulichopanda, ambacho sasa tunakivuna?
Ni nani aliyepanda, na nani anayevuna? Katikati ya hii tafakari, akili yangu inasafiri kurejea hatua za awali za Maisha. Katika hatua ya kwanza ya utoto, jamii inafanya malezi kupitia familia za makundi mawili, familia zenye uwezo mkubwa kiuchumi, na familia zenye uwezo mdogo wa kiuchumi au kwa jina lingine, familia za kinyonge. Kwenye kutafakari, ninaona Watoto wao wakicheza pamoja, wakifurahia na kutaniana bila ya kujali aina ya familia walizotoka. Kiza kinapoingia, kila mmoja anarejea makwao.
Mmoja anaitwa kwa upole na sauti ya kudekeza, mwingine ‘ole wako uwe umechafuka’ inasindikizwa na matusi. Wawili hawa wanahitimu shule ya msingi, mmoja baada ya miaka saba ya vumbi na jasho la kuwahi namba, mzigo wa dumu na fagio. Mwingine baada ya miaka saba ya kutolewa na kurudishwa hadi geti la nyumbani, na safari nyingi za kimasomo kwenye mbuga, vivutio.
Hapa kupungukiwa kunakuwa dhahiri. Mbegu inapandwa. Familia nyonge inajikakamua na kumpeleka kijana wao shule ya bweni. Huko, anakutana na vijana kutoka familia tofauti, lakini yale makundi makuu mawili yanabaki kuwa Dhahiri. Kwenye mfumo wa shule, kuna maduka ya aina mbili, duka ‘dogo’ la bidhaa za bei rahisi ila kwa uchache.
Na kuna duka ‘kubwa’ la bidhaa za bei ya tozo, tena nyingi. Shule ina andaa chakula kwa ajili yao, lakini mezani anafika yule ‘mnyonge’. Mwenzake anaishia dukani kupata vitafunwa na sharubati ya baridi. Mnyonge anatazama yote haya nakujisemea, ‘ipo siku na mimi nita faidi’. Mbegu inachipuza kimea na mzizi.Vijana wote wawili wanahitimu kidato cha sita kwa ufaulu na kudahiliwa kuingia chou kikuu.
Mnyonge anajikimu kwa fedha ya mkopo wa elimu ya juu. Fedha ambayo inabidi afanye ‘juu chini’ itosheleze matumizi yake yote ya muhula mzima, imsaidie endapo atapata dharura yoyote na pia ajitahidi kutenga akiba kutoka kwenye fedha hiohio. Kijana ‘mnyonge’ anakuwa mtu wa kujibana, kujinyima na kama mtume Paulo, anajifunza kudhiliwa na kuona njaa. Upande wa pili, kijana mwenye uwezo au kwa jina lisilo rasmi ‘wakishua’, yeye anapokea fedha yake ya kila mwezi.
Inamtosha kujikimu kwenye chakula na mahitaji binafsi, pia anatenga kiasi tosha kwa ajili ya ‘kuweka shida chini na mikono juu’ kila iitwapo ijumaa. Simu moja nyumbani, ukame unakata. Mnyonge akitazama haya yote, anajawa na hasira juu ya hali yake. Anachukia alipotoka na kuahidi kuwa siku akipata ‘upenyo’ au cheo kikubwa kwenye ofisi kubwa, taasisi, uongozi wa ngazi ya taifa ata hakikisha analipa machungu yote na dharau alizopitia. ‘ipo siku yangu tu!’.
Yule wa ‘kishua’ anaishi vizuri, lakini naye pia anatamani Maisha ya anasa na starehe yasikome. Anatamani Maisha yawe mazuri na mepesi Zaidi, atembelee lile prado vx. Anatamani yale majumba makubwa anayoyaona kwenye filamu na mali nyingi Zaidi. Naye anajitia moyo, ‘ipo siku yangu tu!’.
Akipata ‘upenyo’ hatazembea.Vijana hawa wawili, kutoka mazingira tofauti, na hali tofauti, wana kua, wakibeba lengo moja, kujinufaisha panapo nafasi au fursa. Na endapo wakapata nafasi kwenye vyeo au uongozi watahakikisha wanafanya waliyo dhamiria. Mti unazaa matunda. Mizizi ya ubinafsi katika uimara wake, imefuta kabisa aibu na kufanya ufisadi, ubadhilifu kuwa jambo la kawaida.
Mizizi hii haibagui pa kuota, kwa aliye dhiki na alie navyo, kote panachipua. Na hii ndo changamoto inayokabili utawala bora. Kila anayepata nafasi ya uongozi au cheo kwenye taasisi anawaza kurejeza alicho poteza, kufuta machozi na kulipa kisasi juu ya ile dhiki alioishi nayo miaka mingi au kuendeleza na kuongeza Maisha ya kifahari aliyokuwa akitamani.
Hatima ya utawala bora ina amuliwa na aina ya watu wanao lelewa kwenye jamii na hatimae kushika nafasi za uongozi na vyeo.Licha ya swali la kuvuna, kuwa na jibu moja ambalo ni jamii kwa ujumla, swali la nani mpanzi wa mbegu ya ubinafsi halina jibu moja. Familia zimepanda, jamii imepanda, mifumo ya uendeshaji shule imepanda na hatimae, matunda yake ni jasho la mtu mmoja kufutwa kwa gharama ya machozi ya wengi. Ambao watakuwa wahanga wa uchumiaji tumbo na wizi wa fedha zilizopaswa kuwasaidia wao.
Jawabu la haya yote, ni kushughulikia mizizi, isiote na kisha kuzaa matunda. Siwezi nikahitimisha kwamba kila taarifa ya wizi, ubadhilifu au matumizi mabaya ya fedha za umma yana chanzo kimoja tu cha ubinafsi uliotokana na dhiki au tamaa. Sababu nyingine zipo, lakini kwa asilimia kubwa sana, sababu hii inasimama kama sababu kuu.
Je, kelele hizi zina maana? Je, atatokea mtu mmoja wa kuzingatia na kutilia maanani? Je, kuna tumaini la kuboresha uadilifu kwenye maofisi katika ngazi zote za utawala? Binafsi, sijui! Ila nnachojua kwa uhakika, chakula kinapoa. Nina amua kukatisha tafakari, na taratibu najongea mezani. Siwezi kubali kukosa vyote, utulivu wa akili na chakula.

Upvote
1