Mjadala huru! Ni sekta ipi inayoendeshwa na Serikali inafanya vizuri?

Serikali imefanikiwa Sana kwenye magereza.

Weekend moja tu ukiwa magerezani unakua umeelewa somo.
 

Trafic kukusanya fine
 
Kazi ya serikali sio kufanya biashara,lazima mambo yaende hovyo.
Pole sana tena sana.

Ungejua China kafikia hapo alipo kwa serikali kufanya biashara.

Huo ujinga wa kubinafisisha kila kitu baadhi ya nchi za ulaya wanajilaumu.

Mi sikubaliani na mpango wa Mama, nitaupinga siku zote hata kama ukifanikiwa kwa sababu siyo sustainable.

Leo hii ukikichafua NMB akiondoka muwekezaji bank inakufa.

Namshauri Mama awe na uzalendo kama wa Dkt Magufuli, tusikalili njia za maendeleo kama za ulaya bali tuangalie mazingira yetu, ni afadhali hela wanazoiba akina Mwigulu au akina Nape maana wataziweka Tanzania na zitakuwa kwenye mizunguko lakini ukileta muwekezaji atakuwa anazihamisha
 
KAKA UMWNENA VEMA,SIKUPINGI,ILA NIIJUAVYO BANDARI TUKIIWWKEA MBIA TUMEKWISHA.

HAKUNA MWAKA HATA MMOJA BANDARI HAIPELEKI RUZUKU. SECTOR ZINGINE NAKUUNGA MKONO.

ILA UMESAHAU TANESCO. HUKO NDO PAKUTAFUTIWA MBIA,NA WALA SI MBIA NI MAKAMPUNI YAPEWE FURSA YA KUGAWIA UMEME WANANCHI.

LA BANDARI NITAPINGANA NA WEWE DAIMA. MKIFANYA HIVYO MTACHEKWA.

NIONYESHE MFANO MMOJA TU WA BANDARI KUBWA ILIYOTAFUTIWA MBIA . KATIKA BANDARI ZA BAHATI KUU.
 
Ina maana hujui tatizo la hii nchi ni nini au unataka uambiwe alafu uite watu timu pinga pinga FC.
 
Ina maana hujui tatizo la hii nchi ni nini au unataka uambiwe alafu uite watu timu pinga pinga FC.
Tatizo kuu ni hili
Tunaweza kuanzisha miradi mingi ila hatuwezi kuiendesha na kuitunza kwa muda mrefu
 
Kikubwa ni nchi kupata mapato stahiki!

Kama mwekezaji akiwa analeta mapato mengi kuliko tunavyopata sasa shida iko wapi?
 
Bandari za New York, Singapore na Rotterdam zinaendeshwa na private sector hasa kwenye upande wa operations!
 
"5. Viwanja vya mpira mikoa yote ukiwemo uwanja wa Taifa. Hii nayo haifai iko hovyo kwenye hali mbaya kupindukia"

Mkuu, hilo kuhusu viwanja vya michezo, karibu vyote ni vya CCM.

Ijapokuwa vilijengwa na wananchi kwa kushirikiana na serikali, CCM iliamua kuvichukua vingi kama mali zake binafsi.
 
Vitambulisho vya NIDA
Hili ni janga jingine pia.


Wanaweza kufanya kaz kwa ufanisi kwenye vitambulisho vya mpiga kura tu maana wanajua vinawapa kula matunda ya nchi
 
Viwanja vya mpira mikoa yote ukiwemo uwanja wa Taifa. Hii nayo haifai iko hovyo kwenye hali mbaya kupindukia. Uwanja wa a Taifa ndo hadi watu wanakojoa kwenye masinki ya vyoo!
Hivi vilitakiwa kuwa mali ya umma ila chama dola walijimilikisha tu kihuni.
 
Hivi vilitakiwa kuwa mali ya umma ila chama dola walijimilikisha tu kihuni.
Hi vizuri kuonesha huo uwezo wako kwa kujibu swali uliloulizwa!

Kushindwa kujibu swali ni kielelezo tosha kuwa huna uwezo wowote ule!
 
Wewe utauza mpaka urithi wetu (hifadhi za taifa zote), Kinapa, Ngorongoro n.k

Mungu atuepushe na mtu wa dizaini yako.
 
Hi vizuri kuonesha huo uwezo wako kwa kujibu swali uliloulizwa! Kushindwa kujibu swali ni kielelezo tosha kuwa huna uwezo wowote ule!
Ungekua umeuliza swali usingejijibu mwenyewe mwishoni.

Halikuwa swali hilo ila ni sehemu ya hoja ya kuhalalisha ubia wa kuendesha bandari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…