Mndengereko
JF-Expert Member
- Mar 24, 2011
- 7,296
- 3,398
Heshima kwenu wakurungwa.
Katika kipindi cha miaka 8 iliyopita katika nchi yetu pendwa ya Tanzania kwa maana ya awamu ya 5 na ya 6 tumeshuhudia viongozi mbalimbali wakiteuliwa na mamalaka, hasa mamlaka ya Rais na pasi na kupita muda mrefu viongozi hao ama hubadilishwa vituo vya kazi, ama wengine hutenguliwa uteuzi wao kabisa, pasi na shaka hii ni kutokana viongozi hao kushindwa kuleta matokeo yaliyoyatarajiwa, na kiukweli hili limekuwa likiipa taifa hasara kubwa kwani uteuzi wowote mpya una gharama zake za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
Mifano ya uteuzi ambayo imefanywa na kutenguliwa ipo mingi sana kuanzia ngazi za uwaziri mpaka ukurugenzi wa Halmashaur, mfano wa hivi karibuni ni aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Sumbawanga bi Jane Nyamsenda ambae aliteuliwa tarehe 25-01, 2023 na tarehe 09-03-2023 Uteuzi wake umetenguliwa, kwa kuteuliwa ndugu sixtus mapunda, bahati mbaya ni kuwa mamlaka inapofanya uteuzi au utenguzi haibainishi sababu, hivyo wote tunaishia kuhisi pengne sababu itakuwa ni hii na hii, ila kitu ambacho tunaweza kukubaliana pamoja ni kuwa sababu kuu ya utenguzi ni mteuliwa kushindwa kuleta matokeo au matarajio chanya, hivyo lengo la makala hii ni kupendekeza mawazo mbadala ambayo yatasabisha kupata wateuliwa sahihi(rationale/perfect appointee) ili kulipepusha taifa na teuzi za mara kwa mara
1-Uwepo leadership inventory system/data -hii inaweza kusaidia kupata watu sahihi katika sehemu sahihi kwani kupitia uwepo wa inventory itapeleka taarifa za possible appointee na existing leader kuwekwa pamoja, na hivyo mamlaka inapotaka kufanya uteuzi inakuwa na sehemu sahihi ya kufanya rejea, katika inventory hii taarifa mbalimbali za wahusika zitawekwa ikiwemo taarifa binafsi, taarifa za wenza,academic na work experience, pamoja na career development, halikadhalika kwenye invetory hiyo hiyo pia zitawekwa taarifa za major accomplishment za wahusika, major strength na major weakness zao, hizi taarifa zote zitasaidia kujua wapi appointee ni bora na wapi si bora anahitaji kuongezewa ujuzi, au awekwe wapi(sekta) ambapo udhaifu wake hautaathiri utendaji wa kazi, kitu muhimu cha kuzingatia hapa ni watendaji wa taasis hii (leadership inventory system /data) ni lazima wawe waadilifu na waaminifu na ikiwezekana ufanyaji kazi na uwepo wao uwe ni wa siri kwani baadhi ya wanufaika (possible appointee) wanaweza kutaka kuhonga ili data zao zichakachuliwe katika namna itakayopendeza mamlaka
2-Kuandaliwa kwa possible(potential) appointee-kila mtanzania ana haki ya kuwa kiongozi na mtumish wa umma lakini ni ukweli usiopingika sio kila mtanzania anafaa kuwa kiongozi,kwa mawazo na maoni yangu kiongoz bora ni lazima awe ameandaliwa na awe amejiandaa yeye mwenyewe in advance ,hii itaepusha kiongozi anapokuja katika mfumo kukaa muda mrefu kujifunza namna ya kufanya kazi wakati huohuo akisubirwa kufanya maamuzi ya kitaasisi na kiserikali kwa ujumla au kuogopoa kufanya maamuzi kwa waswas kuwa ataenda kinyume na utaratibu uliozoeleka,hili linaweza kurekebishwa kwa anaetarajiwa kuwa appointed kuandaliwa tofauti na sasa ambapo baadhi huteuliwa ghafla wakiwa hawajijui na wakiwa hawajajiandaa,hvyo kupelekea wengne kuja makazini wakiwa na inferiority complex na kupelekea baadhi yao kuperform chini ya kiwango,wengne huchukua muda mrefu kufanya maamuzi kwa kuogopa.,hili linaweza kurahisishwa kwa kuwa na chuo maalum cha kupika viongoz wanaotarajiwa.ili wanapoingia madarakan waact accordingly (sheria,taratibu na kanuni+ubunifu ) ndan ya muda mfup
3-Kuipa kipaumbele internal promotion -hapa namaanisha watumish wa ngazi za chini ambao wana uwajibikaj mzur,wapewe nafas kushika nafas za juu zaidi badala ya kuteuwa completely new person kutoka nje ya system kwani baadhi yao kwa kuwa hawakuwa katika system ya utumish hufanya maamuzi kinyume na utaratibu na wengne huogopa kufanya maamuzi na kuwaachia subordinates wao,kufanya kwa badala yao au huwategemea zaid katika ushaur na mwisho wa siku kunakuwa hamna mawazo mapya yaliyotegemewa hapo awali,mfano uteuzi wa katibu tawala ,kimuundo katibu tawala ndiyo mkuu wa watumish aidha katika wilaya au mkoa,hvyo anapaswa awe role model na msaada kwa watumish wote,uteuzi wa mtu aliye nje ya mfumo kutekeleza majukumu haya lazima iwe changamoto kwani ni nadra kwa ambae hakuwah kuwa mtumish wa umma kujua A-Z ya mambo ya kiutumish,pia hili litasaidia kuwapa morali watumish wa ngaz za kawaida (chini)kuperform zaidi
Naomba kuwasilisha kwa ajili ya mdahalo,na nyongeza ya alternatives,
NB:Lengo la makala hii sio kukosoa au kukejeli maamuzi yaa mamlaka bali kusaidia mawazo mbadala na kuboresha zaid ili mamlaka isiwe inapata shida kwenye teuzi na ipate perfect appointee kila iwezekanapo.