MARTHA MAGAWA
Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujihusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake.
Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si mazuri kwa afya ya wote wawili, hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajali sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hilo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi.[
http://mtembezi]
Mtembezi.com imekuainishia baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa watafanya ngono wakati KE yupo katika siku zake.
MADHARA KWA MWANAUME
1. Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.
2. Maambukizi katika tezi dume (Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.
3. Kuziba kwa njia ya mkojo.
4. Utasa au ugumba.
5. Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.
6. Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji, utelezi au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.
MADHARA KWA MWANAMKE
1. Kupatwa na maambukizi ya viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi, mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID (PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.
2. Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.[
http://mtembezi]
3. Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.
4. Utasa au ugumba.
5. Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.
Source: mtembezi.com