Prof T Johannes Chacha
Member
- Apr 6, 2020
- 16
- 48
Wakati wengi wanakubali kuwa Akili Mnemba (AI) ina uwezo wa kuleta mapinduzi ya viwanda na kuboresha maisha, kuna wasiwasi unaoongezeka juu ya athari za kimaadili na usalama wa maendeleo yake ya haraka.
Tarehe 25/09/2024 itakumbukwa sana katika historia ya dunia kama siku ambayo mabadiliko makubwa yalitokea katika ulimwengu wa teknolojia. Hii imekuja hivi karibuni baada ya kampuni maarufu duniani, OpenAI, inayojihusisha na masuala ya Akili Mnemba kutangaza kuwa inahama kutoka mfumo wa biashara usio wa faida hadi mfumo wa biashara wa faida.
Kumetokea na mabadiliko makubwa pia katika mfumo wake wa uongozi. Kampuni hii ndiyo iliyogundua mfumo maarufu wa ChatGPT ulioleta mapinduzi chanya kwenye teknolojia. Afisa Mkuu wa Utafiti wa OpenAI, Bob McGrew, na Makamu wa Rais wa Utafiti, Barret Zoph, waliacha kazi katika kampuni hiyo siku ya Jumatano (Septemba 25, 2024), saa chache baada ya Afisa Mkuu wa Teknolojia wa OpenAI, Mira Murati kutangaza kuwa ataondoka.
Elon Musk, Mkurugenzi Mtendaji wa Space X na mmoja wa waanzilishi wa Open AI alipinga mabadiliko ya hivi karibuni ya Open AI. Kupitia chapisho la X (zamani, twitter) Musk alisema kuwa: "Huwezi tu kubadilisha biashara isiyo ya faida kuwa faida. Hicho ni kinyume cha sheria."
Mtumiaji mwingine wa X aliyethibitishwa pia anaandika kujibu chapisho la Elon Musk X:
"Kwa hivyo wacha nielezee hii moja kwa moja, OpenAI inaamua kuwa kampuni ya faida sasa. Afisa Mkuu wa Teknolojia, Mkuu wa utafiti, na Makama wa Raisi wa mafunzo na utafiti wote huamua kuondoka siku hiyo hiyo hii inatangazwa. Sam Altman (Mtendaji Mkuu wa OpenAI) anapata malipo ya $ 10.5B (7% ya kampuni) siku hiyo hiyo. Nadhani Sam alifanya kitu."
Nini maoni yako kuhusu haya mabadiliko? Karibu tujadili.
Je unadhani mabadiliko haya yana athari gani katika jamii yetu ya sasa?