Mjadala kuhusu ukomo wa umri wa mgombea rais waahirishwa, bungeni

Mjadala kuhusu ukomo wa umri wa mgombea rais waahirishwa, bungeni

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Spika Jacob Oulanyah ameahirisha mjadala kuhusu ukomo wa umri wa rais hadi wiki ijayo baada ya kuona polisi wengi wamesambazwa kuzunguka jengo la Bunge, maeneo kadhaa ya jiji la Kampala na kwingineko nchini.

Uamuzi huo wa Spika ulitolewa kutokana na ombi lililowasilishwa na kiongozi wa kambi ya upinzani Winnie Kiizahas ambaye alielezea kitendo hicho cha polisi kuwa ni “kulipindua bunge” na mzingiro huo umelenga kuwaaibisha wabunge.

Kulikuwa na fadhaa kubwa Alhamisi asubuhi baada ya polisi kuwatia ndani wanafunzi watano wa Chuo Kikuu cha Makerere na meya wa jiji la Kampala Erias Lukwago wakati ofisi za chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) zilifungwa na polisi kuzuia maandamano yaliyopangwa kupinga kusudio la kuondoa ukomo wa umri kwa rais.

Polisi waliweka ulinzi mkali wa maofisa wenye silaha eneo lote la bunge huku helkopta ikizunguka juu na wabunge walizuiwa kuingia maeneo ya karibu na magari yao likiwemo la spika ambaye alilazimika kuingia bungeni kupitia mlango wa nyuma.
 
Back
Top Bottom