Hili jambo lilianza kama mzaa vile lakini naona linaendelea kuota mizizi
Zamani ilikuwa mtu akiaga Dunia watu hukutana uweka tofauti zao pembeni Kisha hufarijiana ,hula chakula pamoja na kumuombea marehemu pumziko la aman
Lakini kwa Tanzania mambo yameanza kuwa ndivyo sivyo nyakati hizi Watanzania wanakaa wanasubiri Tanzia ya kiongozi yeyote tu ili wapate sababu ya kufurahia 😢
Je kipi kilichowabadilisha watanzania?
Je kama taifa hatuoni sababu ya kuziba ufa huu kabla hatujaangukiwa na ukuta?
Je zipi ni athari za kuendelea kupuuza dalili hizi?
View attachment 3435005