MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Vilikuwepo vitabu ila kanisa katoliki halikuandika Biblia ila waliviunganisha vitabu ili kupata Biblia. Na vipo vitabu vilivyoachwa kujumuishwa kwenye Biblia. Zamani sisi tulikua tunasoma darasani haya Kama somo. Ni muhimu Sana kujua Nani aliandika vitabu vya Kwenye Biblia, aliwaandikia kina Nani na kwanini, je kuna criticism zozote ktk maandishi yake. Yapo mengi mno mtu anatakiwa ajifunze kuhusu Biblia kabla hajaanza kusoma yaliyomo
 
Nisadie kutaja mstari ndani ya bibilia unaonyesha haya unayosema ww
 
Aliyeleta mada nimemwelewa amechokoza tu ili wajuzi waje kutufunza, lakini mpaka sasa nimechoka kusoma wote mliocoment hamna mjualo zaidi mnagusagusa tu.
Kwa kuwa wengi tunahitaji kujifunza kwenye hili, nina ushauri ufuatao:
Kwanza, usimkosoe mtoa mada kwa kumshambulia kama na wewe huna hoja na ushahidi, Martin Luther ni mtu mkubwa Sana duniani, sasa mjadala wake hatuwezi kufanya kwa kuwa na taarifa zisizokamilika,hapa tunafunzana hatupigi story.
Pili, hata unapotoa comment yoyote jivue kwanza imani yako ili uwe huru kupokea na kujifunza kutoka kwa wenzio.
 
Ndugu mambo mengine unaweza kupata hata Google tu. Biblia ni nini? Unajua kazi ya kukusanya maandiko mbalimbali kutoka kwa waandishi tofauti ilianza lini? Mitume wa Yesu na mababu wengine walieneza injili bila Biblia ndio maana utaona baadhi ya barua zao zimejumuishwa kama sehemu ya Biblia. Orthodox walijitenga na Kanisa Katoliki mwaka 1100. Nenda kamuulize padri yeyote wa Orthodox atakwambia ukweli na sababu ya wao kujitoa.
 
kwa hiyo Martin Luther alitoa hivo vitabu 7 na kanisa katoliki likakubali kutumia bible ya luther na sasa hiv wameamua kuvirudisha siyo
 
kwani catholic siyo dini dola pale Italia na Spain, kama ilivo kwa Anglican pale England
 
safi sana mkuu, wewe utakuwa umesoma "Comperative religion"
 
kwa hiyo Martin Luther alitoa hivo vitabu 7 na kanisa katoliki likakubali kutumia bible ya luther na sasa hiv wameamua kuvirudisha siyo
Kanisa halijawahi kuwa na Vitabu pungufu hata siki moja...Toka Kanisa limekusanya Biblia, biblia imebaki hivyo hivyo mpaka leo
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwatendo, fanyeni yote katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa Yeye.”
Matendo ya Mitume 4:2 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
 
umeanza vizuri,ukaharibu mwishoni!
aya ya kwanza uko sahihi,zilizobakia zote umepotosha!
ila kabla ya kuendelea,nenda kasoma zile 95 thesis za luther,halafu uje hapa!
Naomba kwa msaada wa wanachamvi zishushe hapa mkuu
 
Hata kwenye vyuo vikuu vya kiislamu mkuu?
 
Leta hoja sio vioja mama maria she is nobody on this world "mama tuna mini Mimi nawe" alisema yesu karamuni
Man! Are you serious? Mama Maria anakuwa nobody kwa mamlaka yako? Hongera sana, basi labda wewe ndiye mungu mwenyewe!
 
 
ber: 11510"]KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?

Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa katoliki wakati wake, Yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.

Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya MTU. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo WA sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.


Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na Cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi WA kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.

Na ndio maana Leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi WA Mungu hasa HAWA WA kileo wasiojua nhistoria vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.

Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati WA ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo WA majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi ya kujifunza sana Leo hii lakini kwa Leo naishia hapa.

deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.[/QUOTE]
Soma Biblia upate mataifa
Soma Biblia upate maarifa
 
watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa Soma Biblia upate maarifa ya kumjua MUNGU
 
Martin Luther alileta mapinduzi makubwa sana kiiman,

Wakati mwingine huwa najaribu kuangalia ibada za wakatoriki naishia kucheka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…