MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Memory

Senior Member
Joined
Jun 29, 2011
Posts
106
Reaction score
37
MASWALI MBALIMBALI YALIYOULIZWA KUHUSU KILIMO HIKI

Ndugu wana JF,

Naomba kama kuna mtaalamu wa kilimo anisaidie ili nifahamu makadirio ya kiasi cha mavuno ya mpunga katika ekari moja katika kilimo cha kisasa ili tujipange kutekereza sera ya kilimo kwanza!

Naomba pia kufahamu sehemu ambazo unaweza ukapata washauri wazuri wa kilimo cha mpunga ambao si tu wanatumia makaratasi bali wana uzoefu na hii kazi kwa vitendo kwa muda sasa.

Asanteni.
---
---
---
---
---
===

BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU

---
---
---
---
---
---
---
 
Mkuu wewe upo maeneo gani na unashamba au unategemea kukodi mashamba kama unaweza kwenda dakawa kunawanakijiji wanakodisha mashamba na kama utabahatisha kwenye block za iliyokuwa nafco kunawatu hukodisha block zao utapata watala hukohuko.
 
Ni kigumu kinahitaji kujitoa na usimamizi wa kutosha unaweza ukapata gunia 30 kwa eka inategemea unalima wapi unatumia nini na umejitumaje hili ni shamba la watani zangu wapogoro hawa hawtumii mbolea wala planter.
 
Mkuu wewe upo maeneo gani na unashamba au unategemea kukodi mashamba kama unaweza kwenda dakawa kunawanakijiji wanakodisha mashamba na kama utabahatisha kwenye block za iliyokuwa nafco kunawatu hukodisha block zao utapata watala hukohuko

kasopa nashukuru sana kwa msaada wako japo bado nategemea kupata estimates of maximum yield katika ekari moja kama kilimo kimefanyika kitaalam ili nifanya maamuzi ya mwisho ya kujua kiasi/ukubwa wa eneo ninalotakiwa kutafuta.

Ninafanya utafiti wa kupata maeneo ya kilimo kanda ya Ziwa victoria na Mbeya. Jana kuna mtu amenipatia data za Kilombero hivyo nafikiria pia kufuatilia ikiwa ni pamoja na Dakawa kama ulivyoniambia. Haya ni maandalizi ya kazi ya Mwakani.
 
ni kigumu kinahitaji kujitoa na usimamizi wa kutosha unaweza ukapata gunia 30 kwa eka inategemea unalima wapi unatumia nini na umejitumaje hili ni shamba la watani zangu wapogoro hawa hawtumii mbolea wala planter
Chiwa,
Nashukuru kwa ushauri wako ila naomba ufahamu kuwa hakuna kitu kirahisi hapa Duniani na kadri kitu kinapokuwa kigumu kupatikana ndivyo faida kubwa inavyozidi kupatikana. Dhahabu ni ngumu sana kupatikana na ndiyo maana inalipa zaidi n.k.

Tunachotakiwa watanzania ni kufanya kazi kwa bidii zote ili kuongeza vipato vyetu, hii ndiyo siri pekee ya mafanikio. Hata China ya leo imefikiwa baada ya wananchi kujituma katika kazi na biashara na kupata security za mikopo.

Kama ungenipatia analysis ya prifit margin katika kilimo cha mpunga ingenisaidia zaidi lakini kama hoja ni kujituma, hilo lisikupe shaka.
 
Mkuu mimi kwa maono yangu mpunga unalipa sana tu wala usihofu ispokuwa tafuta eneo lenye maji yakutosha yani usitegemee mvua hasakama utapata maeneo ya mkoa wa morgoro ni nzuri zaid kwakuwa huku gharama za undeshaji ni ndogo ukilinganisha na bara.

Na bei pia huku ni nzuri huduma za madawa beipoa na zinapatkana vinginevyo laba uwe na unyeji wahuko nyanza lakini mimi nakushauri utafute shamba sehem za huku hata samani yake ni tofauti na nyanza kila mwaka linapanda marambili mikopo pia inakubalika kiurahisi kama utakim nyaraka zinazo takiwa

Mungu akubariki ufanikiwe ndotoyako mkuu. Memory,
 
Mwaka jana nililima Ifakara ikala kwangu japo nisiwe mnafki sikuweza kusimamia vizuri na resource hazikutosha sana kwa kifupi kulikuwa na uzembe mwaka huu najipanga tena kulima na nimejaribu kufanya gharama za awali ili nione ina kuwaje kama ninavyo kutumia nadhani kwa mchanganuo huu.

Tutawachokonoa wadau watusaidie zaidi kwani nina plan ya miaka mitatu kwa kila mwaka kuongeza eneo na pia nina mpango wa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kwa kuanzisha umoja wao na kupata bei nzuri zaidi
 
Kuna garama za chini za mahitaji hizo huwa zinarudi kwa kila kitu tunawauzia wasaidizi wa shamba kwa mfano umenunua jiko shs 70000 wanfanya kazi inayofanana na hiyo wakati wa kuondoka unawapa jiko japo mimi nimeamua kutoa hizo bidhaa kwa bei nafuu kwa kiasi fulani ili wasiumie sana.
 
Mkuu mbona kuna mapunguf mengi kwenye mchakato wako napia umepanda gunia tatu 3 katika heka 15 ulitakiwa upande gunia4 napia ni aina gani ya mbegu uliyopanda na unaweza kutujuza ni kiasi gani ulivuna kwa sababu haiwezekani ule hasara kwa heka 15 hata iweje labda mpunga ufe ama hukuzingatia mbegu bora nayo pia ni ngumu sana kupiga chini kwa hesabu hata kamaulilima kienyeji basi ungeambulia hata 6m sio ukose kabisa.

Kwa heka 15 matarajio ya mavuno ni gunia30 kwa heka mbegu bora na matunzo usitegemee mvua utaumia mtalam lazima uwe nae Chiwa,
 
Unachosema ni kweli hiyo kwanza ni plan ya mwaka huu bado inamarekebisho sio gharama halisi mwaka jana nililima eka kumi nikapata gunia 22 usiogope ndio ukweli nilitumia kama 2M kwa kilimo chote kuna mambo mengi lakini kubwa ni usimamizi mbovu kwa kumuamini mtu nilivyoenda kwenye mavuno nikakuta aibu yangu.

Lakini mwaka huu sitaki utani mbaya zaidi hata mbegu walinichanganyia kwa wastani kama usimamizi umekwenda vizuri kulingana na mashamba ya majirani umekosa kabisa basi gunia sita kwa heka japo kuna ugojwa wenyeji wanauita kimyanga huo unaweza kula shamba zima.

Nakushauri tafuta fedha ingia utajua vizuri hapa kweye computa hakuna kitu gharama muhimu ndo hizo maelekezo mengine mbele kwa mbele.tuache uwoga.

Hasara inawezekana wako walio panda hekari 100 na kupata gunia mbili acha wali uwe mtamu muhimu ni kufanya na kurekebisha makosa kadri unavyozoea shamba.
 
kasopa,
Thanks kwa ushauri,

Naomba kama una data za maeneo mhimu kwa kilimo cha mpunga katika mkoa wa Morogoro uwe wa kwanza kunipatia hapa ili niweke plan yangu vizuri kwa ajili ya kuyatembelea nikianza na Dakawa kama ulivyo nitajia hapo awali.

Ahsante!
 
Bilashaka mkuu kidogo nipo nje ya eneo nategemea kurudi tareh28 nikifika ntaku pm kama vip twende ukaonane na wenyeji mojkwamoja
Thanks kwa ushauri

Naomba kama una data za maeneo mhimu kwa kilimo cha mpunga katika mkoa wa Morogoro uwe wa kwanza kunipatia hapa ili niweke plan yangu vizuri kwa ajili ya kuyatembelea nikianza na Dakawa kama ulivyo nitajia hapo awali.

Ahsante!
 
Desa la nguvu ili Tz hasa kyela,ifakara,Mangula,mbarali wengi hutumia system ya kumwaga mpunga badala ya kupanda.
 
Mkuu nimejaribu kufuatilia hii kitu nimeona ina tija sana. Nitaenda kuongea na mshauri wangu wa kilimo kuona kama nitaweza kuapply shambani kwangu. Tatizo ni kwamba wataalamu wetu wakilimo wapo outdated sana na vitu kama kama hivi. Wao na internet ni vitu viwili tofauti
 
Hellow wana jf,

Katika kupambana na Hali ya uchumi, ninajipanga kwenda kulima mpunga huko ifakara na Kwa utafiti kidogo nilioufanya nimeona naweza kutumia km sh 350,000/=, Kutoka kukodisha shamba mpaka kuvuna na nakadilia eka moja.

itatoa gunia km kumi na nitahifadhi mpaka bei iwe km 90000 Kwa gunia la mpunga ndipo niuze hivyo eka moja naweza kupata faida ya sh 550000.

Natazamia kuanza na heka hamsini, naomba waliowahi kulima huko wanipe ushauri kwani nataka kuanza kulima kuanzia mwezi wa tisa.
 
Mkuu ni wazo zuri sana hili na mimi ningekushauri utoe kabisa mchanganuo uno onyesha utatumia kiasi fulani na utapata faida kiasi hiki, make unaweza kuwa una ashumu kutumia hicho kiasi ukaja kujikuta kimepanda juu au kimeshuka chini, Na vile vile Usipende sana kuuza mpunga tu.

Cha kufanya ni kujipanga na kuwa na mashine yako unakoboa una gred unapali na kuuza mifuko ya kilo tano hadi 10, ungeweza kufanya hivyo mwaka mzima tatizo linakuja kwamba Watanzania wengi mashamba tuliyo nayo yaani mtu mmoja mmoja haitoshi kulisha hata Kata moja mwaka mzima,

Kwa nchi za wenzetu utakuta mtu shamba lake moja lina tosha kulisha hata mikoa mtatu mwaka mzima hapo ndo inakuwa raha kuweka mitambo yako ya kuprocess kwa sababu malighafi unayo,

OK KAZI NJEMA NA UKIFANIKIWA URUDU KUTUKUZA NA UKISHINDWA NAPO URUDI KUTUJUZA ILI TUTUMIE KAMA CASE STUDY
 
chodoo,

Salaam Chonde,

Nashukuru kwamba umeonyesha nia ya kulima mpunga ila kabla sijatoa ushauri wangu..Ningependa kujua yafuatayo:

1. Ulishawahi kulima mpunga tofauti na ifakara?
2. Unategemea kukodi shamba maeneo gani? Ie mgeta,chita,malinyi
3.Nafasi yako ya kusimamia shamba ikoje?

Maana nina uzoefu kidogo ktk maeneo hayo nadhan ungenijubu basi ningekushaur kadir niwezavyo!
 
John Deer,
kuhusu kulima mpunga Ndiyo kwanza naanza sijawahi lima sehemu nyingine , na maeneo ni kijiji cha namawala, sitakuwa full time shamba lakini naplan kuwa na visit mara mbili kwa mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…