Singo Batan
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 295
- 198
TAHADHARI KWA NEC UCHAGUZI MKUU 2020
Siku za karibuni pameibuka mjadala Mkubwa Juu ya kuenguliwa kwa Wagombea wa vyama mbalimbali.
Pamoja na Ukweli kwamba Kuenguliwa huko kumezingatia ufuataji wa Katiba ya Nchi na Sheria za Uchaguzi, lakini kuna Mtego umewekwa Tume ionekane haitendi haki katika utekelezaji wa majukumu yake kisheria na upande wa pili, Vyama vibebe Agenda hiyo na kuitangaza sana kwamba vinaonewa na Tume.
Maelekezo haya ya siri yanatolewa na Viongozi wa ACT- Wazalendo & CHADEMA ambao waliwataka;
1. Wagombea wa baadhi ya kata na Majimbo kutojaza taarifa zao katika fomu namba 8B kwa Wagombea Ubunge na C kwa Wagombea Udiwani, ikiwa ni pamoja na kujaza majina ya Uongo na Tarehe za kuzaliwa zinazo kinzana na Taarifa za Nida nk
2. Kushindwa kuweka viambata muhimu katika fomu namba 8B na C Mfano Picha, Fomu namba 10 ya Tamko la Mgombea kukubali na kuheshimu Maadili ya Uchaguzi, "pay in slip" ya malipo ya dhamana nk. kujaza Wadhamini feki, Kutopitisha Fomu na. 8 kwa Hakimu ili asaini na mambo mengine.
Maelekezo haya yalitolewa Makusudi ili Wagombea wengi wakishaenguliwa pawepo na taharuki kwa wananchi, hivyo vyama hivi vitapata kura za Hasira kwa kigezo kwamba Tume inashirikiana na CCM kuvionea Vyama tajwa.
Lengo kubwa hapa sio kushinda Urais,Ubunge au Udiwani bali vyama hivi vipate kura nyingi zitakazovipatia Ruzuku.
Na kwakuwa Wananchi wanaaminishwa kwamba vyama vya ACT Wazalendo na CHADEMA vinaonewa, wanaweza wakasusia kupiga Kura hivyo Dunia itafahamishwa kwamba NEC imeharibu Uchaguzi kwa kuipendelea CCM.
Malalamiko mengi yaliyopo sasa ni kuishinikiza NEC ivunje Sheria na kutoa Favour kwa Wagombea waliokosa sifa baada ya kuomba kuteuliwa, Jambo ambalo litaharibu credibility ya TUME.
Mimi ni mwananchi ninayeona hila na mipango ovu ya wanasiasa uchwara. Madhara ya chokochoko hizi sio tu zitadhoofisha juhudi za Tume kufanikisha Uchaguzi Mkuu, bali kuleta chuki na kuzua vurugu nchini mwetu. Hatutaki tufikishwe huko,Tume ya Taifa ya Uchaguzi simameni Imara!