Mjadala Mzito kuhusu neno Benki ama Baki.


Sawa, Kama ilivyo kenya na Jubilee, chama kipya wanachama walewale wa Kanu,
Yaani Msitu mpya nyani Walewale. Tofauti ni Kuwa hata mimi leo nikitaka nachukua kadi ya ccm naingia kwenye siasa ninaweza kuwa yeyote na hakuna mtu atanitenga kwa kabila langu,
Tofauti na hapo kama sio mkikuyu au mkalenjini Wewe ni Kapuku na huna haki ya kuongoza Kenya,
Hapo mmetawaliwa na Familia ya Mkora tangu uhuru.
 
Haha kwa hiyo mbongo mpaka ajue English ni mpaka asomee Kenya au Ulaya!!!....wacha upotoshaji...wabongo wengi tu wanajua kutumia kiingereza na wamesomea hukuhuku kwetu...lugha ya kiingereza wakati mwingine inaathiriwa na lafudhi ya MTU ama wakati mwingine lugha mama na ndicho kinachotokea kwa watanzania wengi.....kuajiri walimu wakenya,waganda na wengine huko ni interest za shule binafsi...kwan mbona taasisi kubwa zaidi ya shule zinazohitaji kiingereza zaidi zinaajiri watanzania...?? Kw
 
Badala ya "I work" mkenya anasema "I wak" ha ha ha..
 
Kati yako na mimi nani kakurupuka
Makosa makubwa sana ya kiuandishi. Yaani ni ujinga wa hali yaju. Sentensi mbili mistari miwili ichangiwe na neno moja!!? Hilo siyo gazeti kijana. Pesa ni moja ya National Identities.
Hii yako inaitwa 'tunnel mindedness' from "tunnel vision"! Noti zimejaa art and graphics, mfano upande wa mbele ya noti zote za Tz thamani imeandikwa kwa font size tofauti...
Juu ni 10 000 chini ni 10 000
namba ya iyo noti inaanzia font size ndogo inaishia kubwa... F L 1 6..
Kwa huo mtazamo wako haya yote ni makosa?!
Stop being so uptight! Just have an open minded approach to things.
 

Narudia tena, maana naona hatuelewani, kufundishwa lugha shuleni sio issue, lugha yoyote ile unaweza ukafundishwa, ila ili uwe bora kweye kuiongea, lazima uitumie kwenye maongezi ya kila siku, huku Kenya tunatumia lugha zote kwenye ofisi zetu na nyumbani,
Watoto wangu hapa huwa tunabadilisha badilisha, mara Kingereza, Kiswahili na hata kilugha cha asili (maana hatutaki kupoteza lugha zetu za asili).
 
Kipi kinatumika zaidi? English au Swahili??
 
Kipi kinatumika zaidi? English au Swahili??
Kiswahili kinatumika zaidi hasa mtaani, lakini kingereza kipo sana ofisini na hata nyumbani, maana lazima uwe mjanja wa lugha zaidi ya moja dunia hii, pia lugha zetu za asili tunazitumia sana maana ni utumwa kutelekeza asili yako.
 
Ahaaa haaa haaa
Siyo kila KAMUSI ya kiswahili ni sahihi. Kimataifa, taasisi peke ambayo imechapa KAMUSI KUU YA KISWAHILI ni Taasisi ya Ukuzaji wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nje ya hii taasisi hakuna kiswahili.
Color (American) and Colour (British). Benki Tanzagiza, Banki Kunyaland...tosheka mkuu wacha ubishi.
 
Saaafi kabisa.
TUKI NI KISWAHILI NA KISWAHILI TUKI

Neno BANKI si neno la KISWAHILI.
"Banki" ni neno la kiswahili sanifu kama ilivyo "Benki". Tofauti neno moja ni la kiswahili cha Kenya na jingine ni la kiswahili cha Tanzania. Ni sawa tu na neno "sokoni" la kiswahili cha Tanganyika na "marikiti" kiswahili cha Zanzibar. Au "shule" na "skuli" yote ni maneno ya kiswahili ila moja la Tanganyika na jingine la Zanzibar. Jingine ni "bomba" na "mfereji". Kama una hoja nyingine sema.
 

Hehehe!! Umenikumbusha mbali, kipindi nikiwa Zanzibar kwa ujinga wangu nikaanza kuwarekebisha kwamba waache kutumia 'skuli' maana sio Kiswahili, aisei waliniweka sawa nikatulia.
 
Kiswahili kinatumika zaidi hasa mtaani, lakini kingereza kipo sana ofisini na hata nyumbani, maana lazima uwe mjanja wa lugha zaidi ya moja dunia hii, pia lugha zetu za asili tunazitumia sana maana ni utumwa kutelekeza asili yako.
Sawa mkuu nimekupata.....mnajua zaidi kiingereza,tunajua zaidi kiswahili
 
Hehehe!! Umenikumbusha mbali, kipindi nikiwa Zanzibar kwa ujinga wangu nikaanza kuwarekebisha kwamba waache kutumia 'skuli' maana sio Kiswahili, aisei waliniweka sawa nikatulia.
Naam ukienda Rome unafanya kama wanavyofanya wao. Hata mimi suala la kuita "bomba la maji" kuwa ni "mfereji wa maji" ilichukua muda kulielewa. Ndio uzuri wa lugha yetu adhimu ya kiswahili huo.
 
Msamehe Mkuu alitaka kuandika BAK 😜😜

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…