Mjadala: Ni ipi dawa ya kutibu maumivu ya jino bila kung'oa?

Man Ngosha

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2012
Posts
219
Reaction score
69

Habari zenu wana JF,

Mimi ninasumbuliwa na maumivu ya jino kwa muda mrefu sasa,nimevulia kwa muda mrefu tatizo hili japo wengi wananishauri niende kwa doctor nikang'oe jino!

Je, kuna dawa yeyote ya kutibu jino bila kung'oa?Saidia mimi,nateseka sana hasa wakati huu wa baridi!

Mbarikiwe sana.

Nawasilisha.
WADAU WENGINE WENYE UHITAJI WA MBADALA WA KUNGOA JINO
Jino linanisumbua sana kwa sasa yaan kama mnavyojua maumiv ya jino usiku hakuna usingizi wala nn utafikiri godoro lina maji. Daah! nilikua nahitaji kujua dawa ya jino tofauti na kulin'goa.


MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI

Changanya unga wa tangawizi,peke la parachichi,mdalasini na pilipili manga,tumia unga huo kupiga mswaki na kusukutua asubuhi na jioni kwa siku saba au 14 kama tatizo ni kubwa sana.
 
Mkuu Man Ngosha najuwa upo ulaya ingawa hujatuambia upo nchi gani dawa ya jino kuuma ni kuling'owa tu hakuna ushauri wowote ule mwengine Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kutumia kitunguu saumu kiponde ponde halafu weka kwenye jino linalouma .au vipande vya ndulele kama tatu vikate kate kisha chemsha vikisha poa kamulia limao moja na dondoshea matone matatu ya mafuta ya taa kwa kutumia unyayo wa kuku kwenye mchanganyiko wako kwenye sufuria yako, chuja vizuri weka mchanyiko weko mahala pazuri ukipoa sukutua kutwa mara tatu kwa siku saba, meno hayatakusumbua.
 
Mimi nipo Tz yetu hii@mzizimkavu,nashukuru kwa advice zenu nzuri, lakn ile ya kutumia ndulele nilishajaribu sema mi nilisukutua mara mojamoja kwa siku 3 tu!!wacha nijaribu hiyo mara 7,na ile ya vitunguu swaumu nitajaribu.

Baraka za Mungu ziwafunike!!
 
Muone Dr Kifimbo anatibu jino bila kung'oa mimi nilishatumia dawa yake ni kweli imenitibu.
 
Asante sana, nimempigia na amenielekeza anapopatikana !
 
Mkuu@Man Ngosha najuwa upo ulaya ingawa hujatuambia upo nchi gani dawa ya jino kuuma ni kuling'owa tu hakuna ushauri wowote ule mwengine Mkuu.

Hii dhana ya kuwa jino likiwa linauma hakuna matibabu zaidi ya kung'oa si sahihi, kung'oa mara nyingi huwa inashauriwa kama matibabu mengine yameshindikana, ukiona jino linauma sana, maumivu yanaanza yenyewe na mara nyingine linakuamsha usiku, tafsiri yake ni kuwa caries (uozo? ) umekwenda chini sana mpaka kwenye sehemu hai ya jino (pulp) ambako kuna mishipa ya fahamu (nerves) na mishipa ya damu (blood vessels), jino liliofikia hatua hii linaweza pia kutibiwa bila kung'olewa, matibabu yake yanahitaji kuuwa mishipa ya fahamu kwenye mizizi ya jino, kwani mishipa ya fahamu ndio inayoleta maumivu, halafu linazibwa, hivyo utaendelea kuwa na jino lako ila hutosikia maumivu sababu mishipa ya fahamu imetolewa, haya matibabu kwa kitaalamu yanaitwa ROOT CANAL TREATMENT
 
Huwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo cha Tatizo. Dawa ni kwenda kwa daktari wa meno ili aone kama limetoboka ili walizibe kitaalam(u?) au lina matatizo mengine ambayo pia yatashughulikiwa kitaalam(u?). Dawa za kienyeji ni tiba ya muda tu.
 
Very Good "Yakuonea" kama ni mtihani ni 100% umeshinda.

Dawa ya jino si kung'oa, unapong'oa ni sawa na ukawa na kidonda mkononi ukaomba kukatwa mkono. Dawa ya jino unaanzia simple restoration up to root canal treatment kutegemeana na wewe mwenyewe unavyokuwa aware na mabadiliko yanayotokana na kuoza kwa jino. Nashauri unaposikia dalili za mwanzo kabisa za maumivu ya jino ni bora ukaenda kwa madaktari wa meno mapema ili upate suruhisho la tatizo lako.

Pamoja daimaaaaa!
 

Hivi huu ni uganga wa kienyeji au ni nini, yaani niweke mafuta ya taa mdomoni na huo unyayo wa kuku ni kwa ajili ya nini?
mimi pia nina tatizo hilo. Naomba ndugu yangu ukipata maelekezo unielekeze tafadhali.
 
Man Ngosha,

Watafute forever products, wana dawa ya kusukutulia meno inauzwa 13,000/- ukitumia hiyo, jina lako itakuwa historia. Kwani uko wapi tukuunganishe na hao jamaa?

Kama uko mwanza, duka lao ni moja tu, lipo PPF gorofa ya tano karibu na mzunguko wa samaki.
 
Teh teh teh ! we utaua watu wewe!
 
Preta kuna dental clinic nyingi zina madaktari wazuri wa meno.
 
dawa ya jino ni kung'oa.


Mkuu hii sio sahihi na niupotoshaji mkubwa kusema dawa ya jino ni kung'oa, nafikiri inaonyesha ni jinsi gani baadhi yetu hatuna uelewa na elimu juu ya afya ya kinywa ( oral health awareness and education). Jino ni kiungo muhimu sana kama kilivyo kiungo chochote katika mfumo wa mwili , hivyo ung'oaji wa meno si jambo linaloshauriwa kitaalamu hata kama jino linauma, kwani kuna taratibu na matibabu mengine yanaweza fanywa ukabakia na jino lako bila maumivu, ung'oaji wa memo usio na mpangilio mara nyingi husababisha madhara kwenye kinywa, mfano mpangilio mbaya wa meno kwenye kinywa (malocclusion) unaweza sababishwa na ung'oaji meno usio walazima, occlusal disharmony inaweza pia kutokea esp. When there is bilateral loss of posterior teeth, and with continued resorption of alveolar bone inaweza sababisha maumivu ya misuli ya uso (Myofacial pain), naomba tuondokane na hii dhana ya kuwa dawa ya jino ni kung'oa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…