Mjadala wa Elimu Live Nkhrumah leo

shule zinazofaulisha zina walimu waliotulia, wameridhika na kazi zao
 
shule ya benjamin mkapa in walimu hadi wenye masters lakini zero kibao, shule zenye walimu wa diploma wanaojitoa na watulia
 
anazungumzia kuwa mishahara kweli ni midogo, kwa kulinganisha na wengine. mwalimu mwenye digrii anaanza na laki tano, bwana mifugo mwenye digrii milioni moja na laki mbili!
 
anawataka wabunge washughulikie mishahara ya walimu, hata hivyo anasema mishahara ya tanzania ni afadhali kuliko baadhi ya shule za kiafrika
 
hapa tanzania asilimia 4 tu ya shule za sekondari ndio inakidhi vigezo vya kuwa shule za sekondari!
 
tuwe na shule za kitaifa, zinazomilikiwa na wizara ya elimu moja kwa moja, sio halmashauri. halmashauri zimiliki shule baadhi zinazochipukia
 
sharti kwanza tutambue tunataka kujenga taifa la namna gani. kamaliza kwa shukrani
 
anaingia prof mkenda. anatambua uwepo wa zitto na mbatia ukumbini. atazungumzia elimu na uchumi
 
hakuna usawa wa fursa katika elimu. usawa na ubora wa elimu ni vitu vyenye uhusiano
 
Jiulize swali Ni watu wangapi wanaushawishi wa sera*Je waziri mtoto wake anasoma shule ambazo zinatungiwa Sera*Mifumo ya Elimu*Shule Binafsi*Shule za Umma*Na shule zisizofuata Mtaala#Prof Mkenda
 
tunazo shule zisizofuata mtaala wa kitaifa
na shule za umma zinazosimamiwa na sera tunazotunga sisi ndizo zinazoathirika, huko wanakosoma watoto wa wakulima
 
kuwa na usawa katika elimu ni kwa ajili ya umoja wa taifa letu
 
kwa mujibu wa mwl nyerere, waliopata fursa za elimu nchini wakati wa mkoloni ni wahaya, wachagga na wanyakyusa, tena wengi wao wakiwa ni wakristo
 
ndio maana leo iko monongono kwamba watu wameajiriwa zaidi wa kabila fulani tu au wa dini fulani tu. hii ni kwa sababu hatuna usawa katika elimu
 
fursa za elimu tanzania zinashabihiana na viwango vya mapato, na hii haileti tija katika uchumi wa nchi yetu
 
anasisitiza, tunapozungumzia suala la ubora wa elimu tusisahau usawa katika elimu
 
mohamed mringo na salum salum, wajumbe wa tume ya pinda wapo
 
sasa ni mbatia kapewa dk. saba. anapongeza walioandaa majadiliano. anakumbuka prof. mosha alivyoanzisha academic freedom, unawaomba wasomo wawe wakweli wasitetee uovu wa aina yoyote katika jamii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…