Nimepata nafasi ya kusoma hiyo hukumu; ni uzembe tu wa petitioners kutoa ushahidi, na pengine wakili wake alaumiwe;
1. Kwamba mtendaji alikamatwa na matokeo feki na Mpendazoe kwenye Amended Petition alisema ana ushahidi wa CD ambao angeuleta Mahakamani, lakini hakuupeleka.
2. Kwamba kuna kijana alikamatwa na mihuri na karatasi za matokeo na angepeleka CD, hakuipeleka mahakani pia.
3. Kwamba Makongora alikamatwa na masunduku kumi, alipeleka gazeti ambalo hata halikumtaja mtu zaidi ya kusema mgombea wa chama fulani; na hata hivyo hakukua na ushahidi uliotolewa mahakani.
Etc! Kwa kifupi ni kwamba hawakuthibitishwa madai yao "beyond reasonable doubts", Na hata yule aliyeamua kesi ya lema hakuwa na ushahidi wa kumvua Lema ubunge; Wakati hukumu ya Lema imejaa mapungufu kibao; hukumu ya Mahanga ni uzembe wa walalamikaji kuwa makini na ushahidi walioupeleka mahakani, inawezekana wakili hakuwa fit kivile.
I humbly submit.