Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Gwiji la siasa za Tanzania, Tajiri, Bilionea na Mfanyabiashara mkubwa wa Kimataifa, Laingwanan, Mtemi Isike ama Aboubakar Mbowe kama anavyojulikana huko Zanzibar, yuko jela kwa mara nyingine tena kutokana na matakwa ya viongozi wa Tanzania, ambao wanamuogopa kutokana na hoja zake nzito za kuchagiza uwepo wa Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi zisizopingika.
Mijadala hii Muhimu kwa mustakabhali wa Nchi haiwezi kuzimwa kwa njia nyepesi kama hii ya kumfunga au hata kumuua Mtu mmoja tu aitwaye Mbowe, haitawezekana abadani, hii ni mijadala ya kitaifa, haiwezi kuzuilika kwa kumshughulikia mtu mmoja au labda kwa kuifuta Chadema, Gari limeisha waka na sasa liko kwenye mteremko linachanja mbuga, Katiba mpya huu ni wakati wake, huwezi kushindana na wakati ukafanikiwa. Never ever! Mbowe aweza kufungwa ama hata kuuawa lakini si rahisi tena kwa wakati huu kuzima jambo hili.
Nawakumbusha Watawala na wanaowatumikisha wakiwemo polisi , kwamba umuhimu wa Katiba mpya hauwezi kupuuzwa kwa vile tu wao hawataki, hii ni kwa sababu uwepo wa viongozi ama hata jeshi la Polisi pamoja na mambo mengine yote ndani ya nchi unatokana na Katiba na si vinginevyo.
Majuto ni Mjukuu